Ugonjwa wa malale
Ugonjwa wa malale (au malale kwa kifupi) ni maradhi yanayosababishwa na vidusia vinavyoambukiza binadamu na mamalia wengine. Vidusia hivi ni wana wa jenasi Trypanosoma kwa Kilatini. Spishi inayoambukiza binadamu ni Trypanosoma brucei ambaye ana nsususpishi mbili: T. b. gambiense (T.b.g.) na T. b. rhodesiense (T.b.r.). Malale ya ng'ombe au nagana yasababishwa na T. brucei na T. vivax.
Malale | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Infectious diseases |
ICD-10 | B56. |
ICD-9 | 086.5 |
DiseasesDB | 29277 13400 |
MedlinePlus | 001362 |
eMedicine | med/2140 |
MeSH | D014353 |
Zaidi ya asilimia 98 ya malale ya binadamu husababishwa na T.b.g. [1]) Kawaida binadamu anaambukizwa kutokana na kuumwa na mbung’o anayechukua ugonjwa huo, naye binadamu akiwa kwenye sehemu za vijijini. Kuanzia katika kiwango cha kwanza la ugonjwa huu kuna homa, kuumwa kwa kichwa, hali ya mwasho, na kuumwa kwa viungo. Hali hizo huanza katika muda wa juma moja hadi majuma matatu baada ya kuumwa na mbung’o. [2] Muda wa majuma hadi miezi kadhaa baadaye kiwango cha pili huanzia na mchafuko, hali mbaya ya kupatana kiwiliwili, kutosikia, na usingizi wa mang’ amung’amu. Mkakati wa utambuzi ni pamoja na utafutaji wa kimelea unaobainika katika damu iliyoganda ama katika majimaji ya kivimbe cha kiowevu kilicho katika mishipa na mianya ya limfu. Mara nyingi sindano ya mgongo inahitajika ili kuainisha kiwango cha kwanza na cha pili cha ugonjwa. Ili kukinga ugonjwa mahututi lazima ufanywe uchujaji umma unaoonyesha dalili zake kwa kufanya upimaji wa damu kugundua kuwepo kwa T.b.g. Kugundua mapema ugonjwa huu kunarahisisha utabibu hasa kabla ya dalili za nurolojia hazijagundulika. Utabibu wa kiwango cha kwanza unatumia dawa za pentamidine au suramin. Utabibu wa kiwango cha pili unahusika na matumizi ya dawa ya eflornithine ama mchanganyiko wa nifurtimox na eflornithine kwa kutibu T.b.g. [3] Angalau melarsoprol inatibu ugonjwa hizo zote mbili, inatumika kawaida kwa T.b.r. pekee kutokana na athari zinazokuja nazo dawa yenyewe. Ugonjwa huu hutokea katika sehemu nyingine za Afrika, kusini mwa Jangwa la Sahara ukihatarisha wananchi wapata milioni 70 wa nchi 36. Hadi mwaka wa 2010 idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa huo ilikuwa 9,000 idadi iliyopungua kutoka 34,000 ya waliokufa mnamo mwaka wa 1990. Hadi leo hii idadi ya wale wanaoambukizwa ni 30,000 miongoni mwao ni 7,000 katika mwaka wa 2012 ni watu ambao wanaishi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Katika muda wa mwaka 1896 hadi wa 1970 milipuko mitatu mikubwa ilitokea kwanza katika Uganda pamoja na Bonde la Kongo (1896 hadi 1906). Halafu miwili katika 1920 pamoja na 1970 iliyotokea katika nchi kadhaa za Afrika. Wanyama kwa mfano ng’ombe huenda wanachukua ugonjwa na wakaambukizwa.
- ↑ (WHO Media Centre 2013 Fact sheet N*259 Trypanosomiasis , Human African Sleeping Sickness June 2013 url=http://www.who.int/mediacentred/factsheets/fs259/en/]]
- ↑ Kennedy, PG (Feb 2013). "Clinical features, diagnosis, and treatment of human African trypanosomiasis (sleeping sickness)". Lancet neurology. 12 (2): 186–94. doi:10.1016/S1474-4422(12)70296-X. PMID 23260189.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ (Lancet2013 Clinical features, diagnosis, and treatment of human African sleeping sickness Feb] volume 12] issue 2] pages 186-192