Uingereza (maana)
ukarasa wa maana wa Wikimedia
Uingereza ni neno linaloweza kutaja maana mbalimbali:
- nchi ya Uingereza (England) katika kusini ya kisiwa cha Britania ambayo ni sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini
- Kisiwa cha Britania (Great Britain) ambacho ni kisiwa kikubwa cha Ulaya chenye nchi tatu za Uingereza, Uskoti na Welisi
- dola la Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland)
- kihistoria ufalme wa Uingereza katika nchi hii hadi kuunganishwa na Uskoti mwaka 1701
- Milki ya Kiingereza iliyojumlisha Ufalme wa Muungano na koloni zake kote duniani
- katika lugha ya kila siku maana yoyote iliyotajwa hapo juu
- Redio Tanzania imependekeza neno moja la "Uingereza“ kwa ajili ya maana yote tatu
- TUKI imependekeza maneno mawili ya Uingereza (kwa nchi pia kwa ajili ya Ufalme wa Muungano) na Briteni (kwa ajili ya kisiwa); lakini "Briteni“ ina matatizo kwa maandishi ya kihistoria na kijiografia kwa sababu inafanana mno na jina la "Brittany“ au "Bretagne“ amabyo ni mkoa wa Ufaransa.
- BAKITA lilipendekeza 'Inglandi' kwa ajili ya England; ila inasema kwamba haitumiki sana
- Makala hii inajaribu kutumia neno la "Britania“ na kusubiri michango ya wanawikipedia.