Tanbihi
Tanbihi (kwa Kiingereza footnotes au endnotes) ni maelezo ya nyongeza kuhusu matini yanayoandikwa ama chini ya kila ukurasa, mwishoni mwa mlango au pia mwishoni kabisa mwa makala au kitabu.
Maelezo ya tanbihi huandikwa nje ya matini inayoendelea ili kurahisisha kazi ya kusoma.
Namba za tanbihi
haririKuwepo kwa matini huonyeshwa kwa kawaida kwa kuingiza namba ndogo inayokaa kidogo juu ya herufi za mstari kama hapa 1. Wakati mwingi kuna pia herufi kama a au namba zinawekwa kwa mabano baada ya neno au sehemu itakayoelezwa (1).
Mara chache kuna alama kama hizi *, †, ‡, §.
Mahali pa tanbihi
haririTanbihi zenyewe yaani maelezo hufuata ama
- kwenye mwisho wa kila ukurasa (ing. footnotes)
- kwenye mwisho wa mlango au sehemu ya matini
- kwenye mwisho wa makala ya jarida au wa kitabu (ing. endnotes)
- mara chache pia kwenye ukurasa kando ya matini
Fomati ya tanbihi
hariri- kurejelea kitabu: hapa tanbihi huonyesha jina la mwandishi, jina la kitabu, mwaka na mahali pa kutolewa (kuchapishwa), namba ya ukurasa au sehemu inayorejjelewa, ikiwezekana pia mchapishaji na namba ya toleo kama kuna matoleo tofauti ya kitabu hiki: ikiwezekana pia na ISBN ya kitabu
- Mfano: Robert Bringhurst (2005). The Elements of Typographic Style (version 3.1). Point Roberts, WA: Hartley and Marks. pp 68–69.
- kurejelea makala ya jarida au gazeti: jina la mwandishi akipatikana, jina la makala, jina la jarida / gazeti pekee, namba katika mwaka kama ipo, tarehe yake, ukurasa kama ipo
- kurejelea tovuti: sawa kama makala, pamoja na URL (kiunganishi / link ya makala), tarehe ilipotazamiwa
Tanbihi katika Wikipedia
haririTanbihi ni muhimu katika Wikipedia kama marejeo na uthibitisho ya ukweli wa habari zilizopo. Zamani hii haikukaziwa sana lakini siku hizi ni lazima. Kila mchangiaji anatenda vema akiongeza vyanzo kwa njia ya tanbihi. Makala mpya zinazopakuliwa bila kutaja vyanzo ziko hatarini kufutwa.[1]
Katika matini ya Wikipedia alama hizi zinafanya tanbihi yaani maneno ya tanbihi huandikwa kati ya <ref> (TANBIHI) </ref> .
Mwishoni mwa makala kiwepo kichwa cha ==Tanbihi== [2] na chini yake alama hizi: <references/> , Tanbihi tunazoandika katikati ya sentensi zitaonyeshwa baadaye hapa penye alama hii ya <references/> .
Tanbihi
hariri- ↑ Wikipedia:Mwongozo_(Kutaja_vyanzo)
- ↑ tusipotumia visual editor
Marejeo
hariri- Denton, William (2014). Fictional Footnotes and Indexes. Miskatonic University Press.
- Grafton, Anthony (1997). The Footnote: A Curious History. Cambridge, Massachusetts: Harvard University Press. ISBN 0-674-90215-7.
- Zerby, Chuck (2002). The Devil's Details: A History of Footnotes. New York: Simon & Schuster.