Ujerumani ya Magharibi

(Elekezwa kutoka Ujerumani wa Magharibi)

Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani ni jina rasmi ya nchi ya Ujerumani tangu 3 Oktoba 1990.

Ujerumani, kanda za utawala wa washindi wa Vita Kuu ya Pili mw. 1946
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani 1949 - 1990

Ujerumani ya Magharibi

hariri

Kati ya 1949 na 1990 ilikuwa jina la dola katika magharibi na kusini ya Ujerumani. Iliundwa katika maeneo ya kanda za utawala wa nchi washindi wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Marekani, Uingereza na Ufaransa.

Dola hili lilijulikana pia kama "Ujerumani ya Magharibi". Wajerumani wengi hawakupenda jina hili kwa sababu katika lugha ya Kijerumani ni jina la kijiografia kwa kutaja eneo la magharibi la nchi hasa maeneo karibu na mto Rhine. Watu wa kusini na kaskazini kama wakazi wa Bavaria au Hamburg hawakujisikia kama "Wajerumani ya Magharibi".

Mji mkuu ulikuwa Bonn.

Kanda la Kirusi la Ujerumani ilikuwa dola la pili katika Ujerumani kwa jina la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani. Baada ya mwisho wa ukomunisti mikoa yake yote yalijiunga tar. 3 Oktoba 1990 na Shirikisho la Jamhuri.