Bonn (jina rasmi: Bundesstadt Bonn mji wa shirikisho la jamhuri Bonn) ni mjii nchini Ujerumani katika jimbo la Rhine Kaskazini-Westfalia (Nordrhein-Westfalen) kando la mto Rhein karibu na Cologne. Kuna wakazi 314,000 kwenye eneo la 141 km².

Bonn

Bendera

Nembo
Bonn is located in Ujerumani
Bonn
Bonn

Mahali pa mji wa Düsseldorf katika Ujerumani

Majiranukta: 50°44′0″N 7°6′0″E / 50.73333°N 7.10000°E / 50.73333; 7.10000
Nchi Ujerumani
Jimbo Rhine Kaskazini-Westfalia
Idadi ya wakazi (2009)
 - Wakazi kwa ujumla 319,841
Tovuti:  www.bonn.de
Nyumba ya ofisi za Wabunge, sasa jengo la UM
Chuo Kikuu cha Bonn

Bonn imejulikana kimataifa kwa sababu ilikuwa mji mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kati ya 1949 na 1990 na makao makuu ya serikali hadi 1999. Bunge pamoja na wizara zote zilikuwepo Bonn.

Baada ya maungano ya Ujerumani cheo cha mji mkuu kilipelekwa Berlin na ofisi za serikali zilifuata. Hadi leo idara za wizara kadhaa bado ziko Bonn.

Bonn iliteuliwa kuwa mji mkuu wa Ujerumani ya Magharibi mwaka 1949 ka sababu mji mkuu Berlin ilikuwa nje ya shirikisho la jamhuri ya Ujerumani ndani ya eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (Ujerumani ya Mashariki). Bonn ilikuwa mji mdogo mwenye historia ya kiutamaduni. Chaguo hili liliondoa mashindano kati ya miji mikubwa katika Ujerumani ya Magharibi juu ya makao ya serikali kuu.

Kabla ya 1949 Bonn ilifahamika hasa kama mji mwenye umri mkubwa ulioundwa kama koloni na Waroma wa Kale. Wakati wa enzi za kati ilikuwa makao makuu ya maaskofu wa Cologne. Katika karne ya 19 ilipata chuo kikuu kilichokuwa maarufu Ujerumani.

Mtungaji wa muziki Ludwig van Beethoven alizaliwa Bonn.

Tangu uhamisho wa serikali na bunge ofisi kadhaa za Umoja wa Mataifa zilifunguliwa Bonn. Nyumba ya Wabunge imekuwa "UN-Campus Bonn" ikiwa na mradi wa United Nations Volunteers (UNV) pamoja na ofisi zinazoangalia mikataba mbalimbali ya UM kama vile Mkataba wa kimataifa juu ya kanuni za kutunza hali ya hewa, United Nations Convention to Combat Desertification (UNCCD)

Tazama pia

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ujerumani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bonn kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.