Ukenekaji

Ukenekaji (kwa Kiingereza: distillation) ni mchakato wa kutenganisha mchanganyiko kiowevu kwa sehemu zake kama sehemu hizi zina viwango vya kuchemka tofauti. Mchakato wa ukenekaji hutumiwa sana katika kemia ingawa si kazi ya kikemia bali ya kifizikia.

Ukenekaji katika maabara:
1. Chanzo cha joto (hapa iko jiko la Bunsen)
2. Chupa
3. Kichwa cha ujenekaji
4. Kipimajoto
5. Kitoneshi
6. Maji ya kupoza yanaingia
7. Maji ya kupoza yanatoka
8. Chupa ya kusanya mkeneko

Mchanganyiko hutiwa moto hadi sehemu moja ya mchanganyiko inapochemka yaani inageuka kuwa mvuke. Mvuke huo hukusanywa katika chombo cha kitoneshi (condenser) ambamo unapozwa na kutonesha hadi kuwa kiowevu tena. Kiowevu hicho huitwa mkeneko (distillate).

Mkeneko kwa kawaida bado ni mchanganyiko lakini ina kiwango kikubwa zaidi ya dutu yenye kiwango cha kuchemka cha chini zaidi. Mchakato wote unaweza kurudishwa mara kadhaa ili kuelekea dutu safi zaidi.

Mifano:

MarejeoEdit


Viungo vya NjeEdit

Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Wikimedia Commons ina media kuhusu: