Ukosefu wa makazi kwa vijana
Ukosefu wa makazi kwa vijana ni tatizo la ukosefu wa makazi kwa vijana ulimwenguni kote.
Muhtasari
haririUkosefu wa makazi kwa vijana ni suala muhimu la kijamii ulimwenguni kote, katika nchi zinazoendelea na nchi zilizoendelea. Katika nchi zinazoendelea, utafiti na uzuiaji umelenga zaidi "watoto wa mitaani", japokuwa katika nchi zilizoendelea, masuala makuu katika utafiti na kuzuia ukosefu wa makazi kwa vijana yanajumuisha kuvunjika kwa uhusiano wa familia, na sababu nyingine inavyosababisha vijana kuondoka nyumbani.[1]"Watoto wa mitaani" pia hujumuisha wakazi wa mitaani ambao hawana makazi.[2]
Ufafanuzi halisi wa ukosefu wa makazi kwa vijana hutofautiana kulingana na eneo. Nchini Marekani, kijana asiye na makazi ni mtu ambaye yuko chini ya umri wa miaka 21 na hawezi kuishi kwa usalama na ndugu yake, na hana namna nyingine kimaisha kama mbadala ulio salama.[3] Nchini Australia, kuna aina tatu za ukosefu wa makazi ambazo ni: wale wanaoishi katika makazi ya dharura (katika makazi ya watu au 'kutumia makazi ya jamaa zao kwenye nyumba za marafiki), wale wanaoishi katika makazi ambayo yapo chini ya viwango vya hali ya chini katika jamii (nyumba za bweni na kambi za misafara).[4]
Watu wasio na makazi, na mashirika ya watu wasio na makazi, wakati mwingine wanashutumiwa kwa tabia ya ulaghai. Wahalifu pia huwakandamiza watu wasio na makazi, kufanya wizi kwa utambulisho wa watu wasio na makazi na ulaghai wa ushuru kwa ustawi wa jamii.[5][6][7] Matukio haya mara nyingi hujenga dhana mbaya kuhusu vijana wasio na makazi.[8][9]
Australia
haririUkosefu wa makazi kwa vijana nchini Australia ni suala la kijamii, linaloathiri vijana wengi nchini humo.Mnamo mwaka 2006, takwimu za serikali ya Australia, yanayolenga watoto wa shule wasio na makazi, ilipata vijana 20,000 wasio na makazi kati ya umri wa miaka 12 na 18. Makadirio mengine yalipata takriban Waaustralia 44,000 wasio na makazi chini ya umri wa miaka 25.
Kanada
haririNchini kanada, ukosefu wa makazi kwa vijana unatambuliwa kama jambo muhimu la kijamii, hata hivyo, hakuna mkakati au tafiti za kitaifa ambazo zimefanyika. Baadhi ya watafiti huzingatia athari za ukosefu wa makazi kwa vijana ambazo zinaweza kutokea kama usagaji, ushoga, na ubadilishaji wa jinsia nchini Canada. Wengine huzingatia mambo mbalimbali ya afya ya kimwili na kiakili miongoni mwa vijana wa canada wasio na makazi.
Marekani
haririNchini Marekani, vijana wasio na makazi ni makundi tofauti tofauti. Watafiti wengine wanadai kwamba takribani vijana milioni mbili huko Amerika hawana makazi.
Athari za kiafya
haririUkosefu wa makazi kwa vijana mara nyingi huambatana na tabia hatarishi kama vile kuwepo kwa ngono zembe pamoja na matumizi ya dawa za kulevya. Hili hutokea kwa kiwango cha juu zaidi kuliko vijana ambao wana hali nzuri ya maisha . Ingawa hatari ya kuambukizwa ni kubwa zaidi kwa vijana wasio na makazi, tafiti zimebaini kuwa ni 46% pekee ndio wamejaribiwa siku chache zilizopita, na kupendekeza kuwa vijana wasio na makazi hawana uwezekano wowote wa kupimwa magonjwa ya zinaa (STI) kuliko wenzao. Historia ya kupuuzwa na vitendo vya unyanyasaji ni ya kawaida kwa vijana ambao hawana makazi, hivyo mara nyingi hawana imani kubwa na watu wazima na watu wengine wenye mamlaka. Watu wazima wanaotaka kuwasaidia vijana hawa walio hatarini watahitaji kuonyesha kuwa ni waaminifu ikiwa wanataka kujenga uhusiano wowote wa kudumu. Jumuiya za utafiti zimeundwa kwa kutoa upimaji wa magonjwa ya zinaa bila malipo. Ijapokuwa ufikikaji wa mahojiano ulibainisha kiwango cha kizuizi ni 40%, tafiti kama hizo zinazotoa upimaji wa magonjwa ya zinaa bila malipo ziliona marudio yakiwa juu kama 98%. Huduma za kina za kiafya zinazopatikana kwa urahisi zitasaidia kushughulikia viwango vya maambukizi ya magonjwa ya zinaa, na matatizo ya kutengwa na jamii kwa idadi kubwa.
Marejeo
hariri- ↑ Stephenson, Svetlana (2001). "Street children in Moscow: using and creating social capital" (PDF). The Sociological Review. 49 (4): 530–547. doi:10.1111/1467-954X.00346. S2CID 143656213. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2017.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Raffaelli, Marcela (1999). "Homeless and working street youth in Latin America: a developmental review". Department of Psychology. Faculty Publications, University of Nebraska. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2017.
{{cite journal}}
: Cite journal requires|journal=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Defining the Problem and the Population - Runaway & Homeless Youth and Relationship Violence Toolkit". Nrcdv.org. Iliwekwa mnamo 17 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "What is Homelessness?". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-09-27. Iliwekwa mnamo 2016-09-25.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help) - ↑ Claire Scott (5 Julai 2016). "Kinahan gang taking advantage of homeless crisis as part of latest fraud scheme". Dublin Live. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kristin Rodine. "Georgia man gets 10 months for perpetrating 'Operation Homeless' fraud in Boise", 5 May 2017.
- ↑ Kevin Wendolowski (2014). "Fighting fraudsters who target homeless in scams". Fraud Magazine (September–October). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-18. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2017.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Nicholas Confessore. "Homeless Organization Is Called a Fraud", 24 November 2009.
- ↑ David Barnett. "Is Begging Just A Scam, Or A Lifeline For Those Most In Need?", 31 October 2016. Kigezo:Cbignore