Ukunjwi
Ukunjwi ni shehia ya Wilaya ya Wete katika Mkoa wa Pemba Kaskazini, Tanzania. Msimbo wa posta ni 75116. Imepakana na shehia ya Bopwe kaskazini kwa mji wa Wete.
Kata ya Ukunjwi | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Pemba Kaskazini |
Wilaya | Wete |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 3,691 |
Shehia hiyo ina vijiji sita ikiwemo kijiji cha Ukunjwi chenyewe, halafu Chanjaani, Buyuni, Raha, Minyenyeni na Chozi.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 3,691 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 2,769 [2] walioishi humo.
Shehia hii ina skuli moja ya serikali yenye jina la Skuli ya Ukunjwi kwa masomo ya msingi na sekondari hadi kidato cha nne. Skuli hiyo imeanzishwa rasmi mwaka 1977 ila ina ukosefu wa nyumba za waalimu ambapo kuwepo kwake ni muhimu kwa vile asilimia 95 ya waalimu wanaofundisha hutoka Gando na Wete. Skuli ina changamoto ya uhaba wa waalimu wa sayansi kwa muda mrefu sasa, tatizo jengine ni utoro wa wanafunzi na mwamko mdogo wa kielimu kwa wazazi na wanafunzi, jambo linalowapa shida waalimu. Skuli hii imepakana na bahari: hiyo huchangia utoro wa wanafunzi pamoja na umaskini wa kipato ambapo wanafunzi mara nyingi huonekana kuchoka wakiwa madarasani na unapowapa kazi za nyumbani hawafanyi ipasavyo.
Marejeo
- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk. 250
- ↑ "Sensa ya 2012, Kaskazini Pemba - Wete DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-04-20.
Kata za Wilaya ya Wete - Mkoa wa Pemba Kaskazini - Tanzania | ||
---|---|---|
Bopwe * Chwale * Finya * Fundo * Gando * Jadida * Junguni * Kambini * Kangagani * Kinyasini * Kinyikani * Kipangani * Kisiwani * Kiungoni * Kiuyu Kigongoni * Kiuyu Minungwini * Kizimbani * Kojani * Limbani * Maziwani * Mchanga Mdogo * Mgogoni * Mjananza * Mlindo * Mpambani * Mtambwe Kaskazini * Mtambwe Kusini * Mtemani * Mzambarauni Takao * Pandani * Pembeni * Piki * Selem * Shengejuu * Ukunjwi * Utaani |
Makala hii kuhusu maeneo ya Pemba bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ukunjwi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |