Ukuta wa picha ni ukuta ambao umejaa picha takatifu na unatenganisha patakatifu na sehemu kubwa ya kanisa hasa katika madhehebu ya Waorthodoksi.

Ukuta wa picha takatifu katika monasteri ya Valaam (Russia)
Ukuta wa picha katika kanisa kuu la Kupashwa habari, Kremlino, Moskow, Russia.
Ukuta wa picha katika kanisa la Stavropoleos huko Bucarest, Romania.

Kwa Kigiriki unaitwa εἰκονοστάσι(-ον), eikonostasion, eidonostasis, yaani panapowekewa picha, kutokana na eikon, picha, na histemi, naweka).

Waamini wanaelekea altare iliyopo nyuma ya ukuta huo, lakini kwa kawaida hawawezi kuona kinachofanyika huko, kwa sababu ni fumbo la imani. Badala yake wanatazama picha hizo zinazoinua mawazo yao kwa Mungu na kwa maajabu aliyowatendea binadamu hasa katika historia ya wokovu.

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri