Ulanzi

pombe inayotengenezwa kwa kutumia utomvu wa mianzi midogo aina ya Oxytenanthera abyssinica ambayo haijakomaa

Ulanzi ni pombe inayotengenezwa kwa kutumia utomvu wa mianzi midogo aina ya Oxytenanthera abyssinica ambayo haijakomaa.

Mianzi inayoanza kukua hukatwa vilele wakati wa majira ya mvua. Utomvu hukusanywa katika chombo. Kiowevu hiki kinaanza kuchachuka mara moja.

Ulanzi unapogemwa kwa mara ya kwanza huwa mtamu kama mtobe au juisi, lakini unapomaliza muda, huwa mkali.

Ulanzi haudumu muda mrefu.

Ulanzi katika utamaduni

hariri

Ulanzi ni pombe ya asili sana kwa Wakinga na Wapangwa, maana ni jadi kwao kunywa ulanzi, na hata watoto wadogo hupewa ulanzi kama juisi. Ulanzi ni pombe ambayo inaheshimika sana, maana hata wanapokwenda shambani, huenda na ulanzi, na kama ukimpeleka mfanyakazi shambani bila ulanzi, huwa anakaidi kufanya kazi, mpaka apewe ulanzi.

Pia, hata katika harusi, sherehe za kimila kama vile kujengea makaburi("mahoka"), mila za kumrudisha mjane nyumbani ("ngotora"), mila za kuabudu miungu, n.k, ulanzi ndio huwa unatumika zaidi ya pombe nyingine.

Viungo vya Nje

hariri