Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO)
(Elekezwa kutoka FAO)
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (kwa Kiingereza: "Food and Agriculture Organzation of the United Nations"; kifupi: FAO) ni kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachopambana na tatizo la njaa duniani.
Inalenga kuboresha uzalishaji na ugawaji wa mazao na vyakula duniani kwa shabaha ya kuboresha hali ya lishe ya watu duniani.
FAO iliundwa tarehe 16 Oktoba 1945 mjini Québec nchini Kanada. Tangu mwaka 1981 tarehe hiyo hukumbukwa kila mwaka kama "Siku ya Chakula Duniani".
Mwaka 1951 makao makuu yalihamishwa kwenda Roma, Italia.
Mwaka 2007 nchi 191 pamoja na Umoja wa Ulaya zilikuwa wanachama.
Shughuli za FAO ziko hasa za aina nne:
- FAO inawasilisha mawasiliano kati ya wataalamu kwenye uwanja wa lishe na chakula. Inaajiri wataalamu wa kilimo, biolojia, misitu, uvuvi na ufugaji. Inaendesha semina na warsha za kimataifa ambako watalaamu wanakutana na kubadilishana habari na mawazo. Tovuti ya FAO inakusanya habari husika na inatembelewa zaidi ya mara milioni kila mwezi.
- FAO inatuma washauri katika nchi nyingi wanaosaidia kupanga sera za kilimo.
- FAO inakutanisha serikali za nchi nyingi katika masuala ya lishe na kilimo.
- FAO inakusanya ujuzi kwa kazi ya kila siku, inaongoza au kushauri miradi elfu kadhaa ya kilimo kote duniani. Pamoja na Mradi wa Lishe Duniani inasaidia pia katika maeneo yenye njaa kwa kuleta msaada wa haraka kwa watu wasio na chakula.
Ofisi za kanda za FAO
hariri- Ofisi ya kanda la Afrika mjini Accra, Ghana
- Ofisi ya kanda la Amerika Kusini na Karibi Archived 7 Oktoba 2009 at the Wayback Machine. mjini Santiago, Chile
- Ofisi ya kanda la Asia na Pasifiki Archived 9 Novemba 2009 at the Wayback Machine. mjini Bangkok, Thailand
- Ofisi ya kanda la Mashariki ya Kati mjini Kairo, Misri
- Ofisi ya kanda la Ulaya kwenye makao makuu ya FAO Roma, Italia
Viungo vya nje
hariri- Food and Agriculture Organization (FAO)
- Tovuti ya FAO kwa Siku ya Chakula Duniani (Kiswahili) Archived 10 Agosti 2011 at the Wayback Machine.
- Fact sheets / features / press releases
- FAO Statistics Division Archived 9 Mei 2008 at the Wayback Machine.
- FAOSTAT website
- TeleFood Archived 6 Julai 2008 at the Wayback Machine.
- World Food Day
- Avian Flu Archived 12 Februari 2006 at the Wayback Machine.