Umma wa Wapanda Baiskeli Dar es Salaam
Umma wa Wapanda Baiskeli Dar es Salaam (kifupi: UWABA au UWABADAR) ni jina la Shirika Lisilo la Kiserikali la umoja wa Wanabaiskeli kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Umma huu unaruhusu mtu yeyote mwenye baiskeli kujiunga nao bila ada yeyote ile.
Dhamira ya Umma
haririMalengo ya Umma ni kama yafuatavyo:
- Kuhamasisha watu wa Dar es Salaam kutumia baisikeli
- Kuhamasisha wanawake kupanda baisikeli
- Kufanya utafiti kupata taarifa kuhusu wapanda baisikeli na maoni yao
- Kushirikiana na serikali na kuhamasisha na kuwashauri kuweka huduma kwa wapanda baisikeli na kuweka mazingira mazuri na salama kwa wapanda baiskeli (mfano sehemu maalumu ya barabara hasa kwa baisikeli, sehemu za kupaki baisikeli, sehemu za kuoga baada ya kupanda baisikeli)
- Kuhamasisha na kuwashauri serekali kuweka mazingira mazuri na salama kwa usafirishaji wa mizigo kwa baisikeli
- Kushirikiana na mashirika mengine ambayo yana malengo kama haya
- Kuhamasisha waendesha magari kuheshimu na kuwapa nafasi wapanda baisikeli na kuwapa haki zao barabarari
- Kuhamasisha wapanda baisikeli kuendesha salama, mfano kutumia taa usiku, kutumia kofia ngumu (helmet) na kujua sheria za barabarani
- Kuwasaidia watu ambao wameumizwa na waendesha magari wakati wa kupanda baisikeli ili kupata fidia zao[1]
Kamati
haririWanakamati wa Umma:
Marejeo
hariri- ↑ "Katiba na Malengo ya Umma". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-26. Iliwekwa mnamo 2009-01-06.
- ↑ "Kamati ya UWABA". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-11-06. Iliwekwa mnamo 2009-01-06.
Viungo vya Nje
hariri- Tovuti Rasmi ya UWABA Ilihifadhiwa 6 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Umma wa Wapanda Baiskeli Dar es Salaam kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |