Upinde (kutoka kitenzi "kupinda") ni mti uliokunjwa na kuunganishwa kwa kamba au ngozi hutumiwa kwa ajili ya kurushia mishale.

Mtu akitupa mshale kwa kutumia upinde.

Historia ya upindeEdit

Inaaminika kuwa upinde wa kale kabisa ulipatikana Holmegård nchini Denmark ukiwa na miaka 8.000.

Upinde ulitengenezwa kwa minajili ya kuwinda wanyama wenye mbio na ambao hawangefikika kwa kukimbizwa mbio au kurushiwa mawe.

Baadaye, upinde ulitumika kama zana za vita jamii zilipokuwa zikikabiliana na maadui zao. Hata hivyo teknolojia hii ya kutumia upinde kama zana za vita imepitwa na wakati kwani kuna zana nyingine zilizo na haraka na bora kuliko upinde na mshale.

Leo upinde hutumika kwa minajili ya kuwinda na katika mchezo wa archery ingawapo wachezaji wa mchezo huo hutumia upinde wenye muundo tofauti na ulioboreshwa

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu: