Mshale (wingi: mishale) ni ala ya vita au silaha ndogo ifananayo na mkuki inayorushwa kwa upinde.

Mishale.

Kwa maelfu ya miaka, watu duniani kote wamewahi kutumia upinde na mishale kwa uwindaji na kwa ajili ya ulinzi.

Historia

hariri

Ushahidi wa kale kabisa wa mshale wenye kichwa cha jiwe ulipatikana Mapango ya Sibudu nchini Afrika Kusini. [1]. Mshale huo unaaminika kuwa ulitumika miaka 64,000 iliyopita.

Ushahidi wa kale kabisa wa matumizi ya upinde kurusha mshale ni wa miaka 10.000 uliopatikana Bonde la Ahrensburg kaskazini mwa mji wa Hamburg, nchini Ujerumani.[2]

Tanbihi

hariri
  1. Lyn Wadley from the University of the Witwatersrand (2010); BBC: Oldest evidence of arrows found
  2. McEwen E, Bergman R, Miller C. Early bow design and construction. Scientific American 1991 vol. 264 pp76-82.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: