Upofu wa rangi
Upofu wa rangi (kwa Kiingereza: "colour blindness") ni ugonjwa unaomfanya mtu asiweze kuelezea tofauti kati ya rangi fulanifulani. Watu wenye ugonjwa huu hawawezi kuona tofauti ya rangi wakati wote.
Kwa kawaida ugonjwa huu ni wa kurithi, wakati mwingine ni matokeo ya uharibifu kwa mishipa ya macho au ya ubongo kushindwa kufanya kazi yake vizuri. Pia inaweza kusababishwa na mgusano na kemikali fulani na macho ya mtu.
Mara nyingi upofu wa rangi ni wa kudumu, yaani hauponi, lakini hali fulani inaweza kusababisha upofu wa rangi wa muda mfupi. Hakuna tiba ya upofu wa rangi wa kudumu.
Inasemekana kuwa upofu wa rangi huwapata hasa jinsia ya kiume kuliko ya kike.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Upofu wa rangi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |