Kemikali
Kemikali (pia: tindikali) ni dutu yenye tabia za kikemia za kudumu iliyoundwa na viwango maalumu vya elementi za kikemia. Elementi hizi haziwezi kutenganishwa bila kuvunja muungo wa kikemia.
Kemikali inaweza kupatikana kama
- elementi tupu, mfano sulfuri safi kando la volkeno
- kampaundi yaani msombo, mfano maji ambayo ni maungano ya hidrojeni na oksijeni
- aloi yaani muungano wa metali mbili au metali moja na dutu nyingine
- mchanganyiko wa dutu kama asidi hidrokloridi ambayo ni mmumunyo wa HCl na maji.
Kemikali zinazopatikana nyumbani hujumuisha maji, chumvi na klorini (buluu).
Tanbihi
haririMakala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kemikali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |