Ups and Downs
"Ups and Downs" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 31 Disemba 2017 kutoka kwa msanii wa muziki wa hip hop kutoka Dodoma, Tanzania, Miracle akiwa na Godzilla. Wimbo umetayarishwa na Bin Laden kupitia studio ya Destination Sound.
"Ups and Downs" | ||
---|---|---|
Kava la Ups and Downs | ||
Wimbo wa Miracle akiwa na Godzilla | ||
Umetolewa | 31 Disemba, 2017 | |
Umerekodiwa | 2017 | |
Aina ya wimbo | Hip hop | |
Lugha | Kiswahili | |
Urefu | 3:16 | |
Studio | Destination Sound | |
Mtunzi | Miracle Godzilla | |
Mtayarishaji | Bin Laden |
Historia
haririKiasili, wimbo ni wa Godzilla, lakini bahati mbaya hakuumalizia. Aliingiza kiitikio tu, ndipo Bin Laden alipoona bora Miracle asababishe katika mpango wa beti. Bin Laden anamwendea hewani Miracle na kumuasa alisibadili maudhui ya wimbo. Bin Laden anamtaka Miracle atunge mashairi yanayoendana na madhui ya kiitikio. Hii inatokana na Bin Laden mwenyewe kumtia sampuli ya biti-korasi na hatimaye Miracle kamalizia mazima. Wimbo ulianza kutengenezwa katika studio ya Godzill - West-Coast huko Salasala, Dar es Salaam, kabla kwenda kumaliziwa kabisa huko Destination Sound ya mjini Dodoma. Hadi mzigo unafika Dom, Miracle alikuwa tayari keshamaliza beti zote mbili za wimbo huu. Wakiwa Dom, Miracle anaingiza kile alichokitunga katika biti, kisha Bin Laden anarudi tena Dar es Salaam, West-Coast. Baada ya kumalizika wimbo, Miracle amekaa kama mwezi hivi ndipo ulipoachiwa rasmi. Video ya wimbo huu imetayarishwa na Kyonaboy kupitia Kyona Media Production. Mchizi Kyona nae anatokea Dodoma, lakini walikutana na Miracle wakiwa DAR na kufanya maangamizi katika video hii. Walifanya video maeneo ya Salasala na Mbezi. Hasa kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Maudhui
haririKwa ujumla wimbo unazungumzia harakati za maisha. Kuna kupanda na kushuka. Ukikumbana nazo, chukulia kama changamoto za mapambano katika maisha. Kuna wanaopenda kufanya wenzao vibonde, umbea, unafiki na mengine mengi.
Ubeti wa kwanza
haririKatika maisha, kuna watu aina mbalimbali. Wapo ambao wao wanapenda kuona unapata maendeleo na kupitia wewe, wanaweza kujifunza mema yako na kuiga maendeleo yako. Wapo visonoko, vichwa maji waliojawa na choyo pale wanapoona unapata mafanikio. Vilevile kuna wale wanaotumia nguvu nyingi kukurudisha nyuma kwa kutumia uwezo wao wa kifedha. Katika ubeti huu, Miracle anaanza na kusema:
Ubinadamu kazi alisema kibla Sir Nature,
Wanataka wakuweke chini kisa wana Pesa,
Wanapenda Life yako isiwe freshi iwe Mbovu,
Mfukoni hauna Cash, kichwani unaStress mobb.
Haitoshi, bado anashangaa na jinsi mtu anavyokesha kukuombea mabaya. Anaacha kuomba Mungu apate pepo badala yake anakuombea weye mabaya ukose maisha ya furaha duniani. Rejea mstari unaosema:
Asa kwanini unaiombea mi MATATIZO MZEE,
Unaacha kumuomba Mungu uende PARADISO MZEE,
Sijui kwanini!! Siku hizi tumekua hatupendanagi
Katika maisha, kuwa na washikaji masnichi ni jambo ambalo humtokea karibia kila mtu. Sio wote wanakuunga mkono asilimia mia moja. Miracle anaona urafiki bora na uhakika unabaki kwa mama aliyekuzaa tu, basi.
Tazama mistari:
Naamini Mama ndo Mshikaji wa kweli ambae atanishikilia hadi kesho,
Sio mshkaji ambae ukizinguananae anakushkia hadi Beto,
Asa kwanini hautulii na maisha yako unahangaika,
Unafatilia maisha ya watu kama we hauna Maisha,
Namaanisha hausomeki sikuelewi niaje,
Mi sina nguvu pambana tu na maisha niache.
Ubeti wa pili
haririUbeti huu umetazama sana namna mtu wa karibu anavyoweza kukuangamiza akiwa huku anakuchekea. Namna nafsi za watu zilivyojawa na choyo. Mtu anasononekea mafanikio yako wakati yeye hafanyi juhudi zozote na anakaa kwao chupi tu hadi anunuliwe na mama, lakini yupo mbele katika kuponda harakati zako. Miracle anaona sio lazima yeye apendwe na mtu wa muundo huo. Tazama mistari kama:
Badala ungoje lini yesu atarudi unangoja nife,
Mi sikupendi Babu hata ukiniletea mambo ya kike,
Acha kusnitch Manigger, hujui hata jins SH ngapi,
Mtoto wa kishua hadi boxer unanunuliwa na B mdashi.
Miracle anadhirisha dhana ya kuwa "maisha ubishi", kujibu mabaya kwa njia ya heri. Kupambana na wajanoko kwa hali na mali. Anamkumbusha mnafiki wake pesa haichimbi kaburi na ubaya hauna kwao. Leo unanifanyia mimi, kesho huenda ukarudi kwako.
Nyota nikishine watabaki macho juu,
Izo tano za kinafki hata usinipe baki nazo tu,
Sioni unachofanya, unanichora picha nafuta,
Muda ambao unapoteza kunidiss mi natafuta,
ongea na watu pesa haichimbi kabuli,
Inazika tabu na kufanya uone mjini pazuri,
Dunia kubwa jiachie acha kunibania.
Halafu Godzilla anamalizia kwa kusema:
Unapigana mpaka soo, mood inakata unadata uko Happy unajihisi uko Down,
Watu wanakuchoraa, kumbe Life ni Ups and Down.
Tazama pia
haririViungo vye Nje
hariri- Video ya "Ups and Downs katika YouTube
- katika wavuti ya DJMwanga Ilihifadhiwa 17 Januari 2022 kwenye Wayback Machine.