Us Against the World
"Us Against the World", wimbo halisi kutoka kwa kundi la Westlife, ni wa pili kutolewa kama single katika nchi Ireland na Uingereza kutoka albamu ya tisa ya kundi hili, Back Home. Hii ilihakikishwa na mmoja wa wanamuziki wa bendi hii Nicky Byrne katika onesho la X Factor wakati akifanya mahojiano na katika wavuti ya bendi hii ya .[1]
“Us Against the World” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya Westlife kutoka katika albamu ya Back Home | |||||
Muundo | CD single, digital download | ||||
Aina | Pop | ||||
Urefu | 4:01 | ||||
Mtunzi | Arnthor Birgisson, Rami Yacoub, Savan Kotecha | ||||
Mwenendo wa single za Westlife | |||||
|
Wimbo huu ulitengenezwa na Arnthor Birgisson, Rami Yacoub na Savan Kotecha. Pia wamechangia katika kutengeneza midundo katika albamu ya Back Home katika nyimbo za "Something Right", "The Easy Way", na wimbo wa "Pictures In My Head".
Wimbo wa ‘’Us Agaist The World’’ pia ulitengenezwa maalumu kwa ajili ya mashabiki wa Westlife kwa ajili ya ushirikiano wao. Kundi hili lilifanya tamasha lao la moja kwa moja la wimbo wa ‘’Us Agaist the World’’ katika kipindi maalumu cha televisheni kinachoitwa ‘’The Westlife Live Show’’ kilichotangazwa tarehe 15 Desemba
Nchini Ufilipino, wimbo huu pamoja na video yake viliongoza katika siku ya jubilee ya kundi hilo ya tarehe 3 july 2008
Orodha ya nyimbo
haririCD ya kwanza
hariri- Us Against The World (Single Mix)
- Get Away (Exclusive B-Side)
CD ya pili
hariri- Us Against The World (Single Mix)
- I'm Already There (Ashanti Boyz Remix)
- Us Against The World (The Wideboys Remix) (Radio Edit)
Nyimbo za Video
haririKundi hili lilitangaza katika wavuti, kuwa utengenezaji wa video tarehe 4 Desemba mwaka 2007, [2] video ya muziki huu ndio ingekuwa moja ya hatua nzuri katika historia ya kundi hili.
Video hiyo iliongoza tarehe 14 mwezi wa pili wakati single yao ilipotoka rasmi tarehe 3 march 2008.[3].
Hatua za kwanza katika utengenezaji wa video hii, unawaonesha vijana hawa wakiwa na wapenzi wao ambapo video hii ilifanyika katika uwanja wa Twickenham Rugby Stadium katika jiji la London kwa kipindi cha wiki siku mbili Louis Walsh, ambaye yeye ni meneja wa kundi hili, alishika nafasi ya kuwa kama sanamu katika video ya wimbo huo. Hata hivyo kundi hili liliweza kutengeneza video nzuri zaidi baada ya Simon Cowell kukataa video ya hapo awali, nah ii inaweza ikawa ndio sababu ya kusogezwa mbele kwa tareye ya kutoka kwa video hiyo kutoka tarehe 3 march hadi tarehe 25 Februari
Video inaonesha wanamuziki wa kundi hilo wakiwa katika zulia la rangi nyekundu ndani ya gari linaloendeshwa, na wapenzi wao wakiangalia picha zao za zamani
Kutolewa na mtiririko wa matamasha
haririTangu kutoka kwa wimbo huu, umefanikiwa kushika nafasi ya arobaini katika chati ya muziki ya nchini Uingereza, na pia ulishika nafasi ya ishirini na saba (27¬) katika chati ya muziki ya nchini Ireland.
Tarehe 3 Machi 2008, single hii ilitolewa katika hali halisia, na kuweza kutoka katika nafasi ya 32, hadi nafasi ya 8 katika chati ya single ya Uingereza, na kushika nafasi ya 6 katika chati ya single ya nchini Ireland. Wimbo wa moja kwa moja kutoka katika single hii, umekuwa ndio wimbo pekee wa kutoka kwa Westlife kushindwa kufika katika nafasi ya tano katika chati ya muziki ya Uingereza, na hivyo kuufanya wimbo wa "Us Against The World" kuwa wimbo uliowahi kupata nafasi ya chini zaidi hadi hii leo. Katika chati ya muziki ya Marekani wimbo huu pia ulifanikiwa kufika hadi nafasi ya 14 na nafasi ya 24, katika chati ya Uingereza
Chart | Ilipata nafasi |
---|---|
Irish Singles Chart | 6 |
UK Singles Chart | 8 |
Single hii ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika chati mablimbali za redio nchini Ireland, ingereza na Vietnam, Afrika ya Kusini na Ufilipino. Na kufanikiwa kushika namba 2 katika nchi yza Thailand, namba 7 katika nchi ya Indonosia na namba 20 nchini Sweden wakati nchini Rusia ikishika nafasi ya 22.
Marejeo
hariri- ↑ Westlife's Next Single Archived 24 Juni 2008 at the Wayback Machine. Westlife.com
- ↑ 'Us Against The World' Video Shoot News Archived 24 Juni 2008 at the Wayback Machine. Westlife.com
- ↑ 'Us Against The World' Single Order Amazon.co.uk