Usangi ni sehemu ya kaskazini mwa Upare ambayo inajumuisha Usangi na Ugweno - kaskazini mwa Tanzania.

Usangi iko kati ya Ugweno kaskazini na Mgagao kusini mwa Upare. Upande wa magharibi inapakana na Mwanga, makao makuu ya sasa ya kiutawala ya Wilaya ya Mwanga, na upande wa mashariki unaunda mpaka wa Tanzania na Kenya.

Usangi iko kwenye safu za milima ya Upare inayoelekea kwenye mlima wa Kilimanjaro upande wa kaskazini.

Usangi ulitawaliwa na watawala wa Kisangi walioitwa Wafumwa (Fumwa likiwa mzizi wa neno. Watawala hao alianza ni Mfumwa Sangiwa Makoko aliyefariki mwaka 1881 hadi Mfumwa Shabani Mtengeti Sangiwa aliyetawala mpaka mwaka 1962 ambapo utawala wa kimila ulifutwa kufuatia uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.

Ufalme huo ulitawaliwa kwa muda mfupi na mtawala asiyekuwa Msangi, Mfumwa Sabuni, kabla ya Wasangi kuurejesha utawala huo na Mfumwa Shabani kutawazwa.[1]

Marejeo

hariri
  1. [1]