Utekaji nyara wa Gumsuri

kijiji cha Gumsuri

Utekaji nyara wa Gumsuri ulitokea mnamo Desemba 13 mwaka 2014, ambapo takribani wanakijiji 172-185 katika kijiji cha Gumsuri walitekwa nyara, wakishukiwa kutekwa na Boko Haram. Watu 32-35 waliuawa.[1] [2] [3]

Utekaji nyara na mauaji

hariri

Wanajeshi hao walifika kijijini kwa malori usiku. Walipofika huko, walikivamia kijiji hiko kutoka pande mbili tofauti. Kwanza walianza kuwapiga risasi wanaume, wakiwaua na wavulana wakubwa mbele ya familia zao. [4] Kabla ya kuwapiga risasi, washambuliaji hao walipiga kelele kwa kusema maneno "Allahu akbar", ambayo yanatafsiriwa kuwa "Mungu ni mkuu". [5] [6] Baada ya hapo, walianza kuelekea wanawake na watoto. Wanajeshi hao wenye silaha waliteketeza nusu ya kijiji na mabomu ya petroli. Washambuliaji hao waliwachukua wanawake na watoto wanaoishi katika kijiji mbali na malori yao. [7]

Baada ya utekaji nyara na mauaji

hariri

Licha ya utekaji nyara na mauaji kutokea tarehe 13 Desemba, habari hazikuibuka hadi tarehe 17 Desemba kwa sababu washambuliaji hao waliharibu minara ya mawasiliano katika eneo hilo. Habari za tukio hili ziliibuka wakati manusura kutoka kijijini hapo walipowasili katika jiji la Maiduguri, ambapo waliweza kuwasiliana na wengine kuhusiana na habari za kile kilichotokea. [8]

Uokoaji wa kijeshi

hariri

Mnamo Aprili 2015 jeshi la Nigeria liliokoa idadi kubwa ya mateka wa Boko Haram kutoka Msitu wa Sambisa, wakiwemo wale waliotekwa nyara kutoka Gumsuri.[9] Walionusurika waliripoti kwamba baadhi ya wanawake na watoto walikufa wakati wa miezi yao ya utumwa; wengine waliuawa wakati wa kazi za kijeshi.[10]

Itikio/Matokeo

hariri

Marekani ilitoa maoni kuhusu utekaji nyara, ikisema, "Tunachukia vurugu kama hizo, ambazo zinaendelea kuleta athari mbaya kwa watu wa Nigeria, na tunatoa pole kwa wahasiriwa na familia zao."[11]

Marejeo

hariri
  1. C. L. Stanley (2000). "How well do we take care of our people?". PsycEXTRA Dataset. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
  2. C. L. Stanley (2000). "How well do we take care of our people?". PsycEXTRA Dataset. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
  3. C. L. Stanley (2000). "How well do we take care of our people?". PsycEXTRA Dataset. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
  4. "Boko Haram freed Nigerian women tell of captivity horror", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2015-05-04, iliwekwa mnamo 2021-06-26
  5. C. L. Stanley (2000). "How well do we take care of our people?". PsycEXTRA Dataset. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
  6. C. L. Stanley (2000). "How well do we take care of our people?". PsycEXTRA Dataset. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
  7. C. L. Stanley (2000). "How well do we take care of our people?". PsycEXTRA Dataset. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
  8. C. L. Stanley (2000). "How well do we take care of our people?". PsycEXTRA Dataset. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
  9. C. L. Stanley (2000). "How well do we take care of our people?". PsycEXTRA Dataset. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
  10. C. L. Stanley (2000). "How well do we take care of our people?". PsycEXTRA Dataset. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.
  11. "United States Condemns Suspected Boko Haram Attack In Gumsuri". Channels Television. Iliwekwa mnamo 2021-06-26.