Uwanja wa Taifa (Tanzania)

Uwanja wa Taifa wa Tanzania unajulikana pia kama Uwanja wa Mkapa ni uwanja wa michezo unaopatikana nchini Tanzania katika mkoa wa Dar es Salaam.

Uwanja wa Taifa (Tanzania)

Uwanja huo. uliojengwa karibu kabisa na uwanja wa uhuru, uwanja wa zamani wa taifa wa Tanzania, ulifunguliwa rasmi mwaka 2007.

Uwanja huo unatumika pia kwa ligi kuu ya mpira wa miguu pamoja na sherehe au matukio mbalimbali ya Kitaifa na yasiyo ya Kitaifa.

Ni moja ya viwanja vikubwa vya michezo barani Afrika ukiwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 60,000 na pia ni uwanja mkubwa zaidi wa michezo nchini Tanzania, uwanja huu ulijengwa na kampuni ya wachina ya Beijing Construction Engineering Group kwa gharama za dola za kimarekani milioni 56.

Mechi ya mwanzo mwanzo katika uwanja huu ilikuwa ni kati ya Simba S.C. na Young Africans S.C.[1]

Marejeo