Uwanja wa michezo wa Aleksandria

Uwanja wa mpira wa miguu

Uwanja wa michezo wa Aleksandria (Kiarabu إستاد الأسكندرية) ni uwanja wa michezo wenye malengo mengi katika wilaya ya Moharram Bey ya Aleksandria nchini Misri. Ulijengwa mnamo mwaka 1929 na Mfalme Fouad, unachukuliwa kuwa uwanja wa zamani kabisa huko Misri na Afrika yote. Uwanja wa Alexandria sasa una uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 20,000 baada ya ukarabati mnamo mwaka 2016-2017.[1]

Uwanja wa michezo wa Alexandria

Uwanja huo unashikilia timu ya mpira wa miguu ya Al Ittihad Alexandria Club | Al-Ittihad na umekuwa uwanja wa mashindano mengi ya kimataifa, pamoja na uzinduzi wa Michezo ya Mediterania mnamo mwaka 1951.Ulikuwa ukumbi wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1986 na Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2006, na uliandaa mechi za Kundi B wakati wa Kombe la Afrika la mwaka 2019 | Kombe la Mataifa ya Afrika la mwaka 2019.[2]

Usanifu

hariri

Uwanja huo ulibuniwa na Mrusi mbunifu Vladimir Nicohosov, ambaye alishawishiwa na usanifu wa Kiislamu.[2]

Viungo vya nje

hariri

Marejeo

hariri
  1. البطولة العربية.. ما لا تعرفه عن استاد الإسكندرية Archived 29 Julai 2017 at the Wayback Machine. البوابة نيوز
  2. 2.0 2.1 "Exploring the History of Stadiums and Egypt's Three Oldest AFCON 2019 Venues". Egyptian Streets (kwa American English).{{cite web}}: CS1 maint: url-status (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Aleksandria kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.