Uwanja wa michezo wa Oppenheimer

Uwanja wa michezo wa Oppenheimer ni uwanja wa mpira wa miguu ulioko huko Orkney, nchini Afrika Kusini. Hapo awali ulikua ukichukua takribani watu 23,000; lakini hapo baadaye uliongezwa ukubwa na kuweza kuchukua watu 40,000 wakati wa kombe la Dunia la mwaka 2010. Jina la uwanja huu liitokana na jina la Harry Oppenheimer, ambaye ni mtoto wa Ernest Oppenheimer na mwenyekiti wa zamani wa De Beers. Mnamo Januari 13, mwaka 1991, wakati wa mchezo wa mpira wa miguu wa "kirafiki" kati ya Kaizer Chiefs na Orlando Pirates, kulitokea vifo 42, kutokana na watu kukanyagana na kuripotiwa kama tukio la pili baya la michezo nchini Afrika Kusini.

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Oppenheimer kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.