Uwanja wa Ndege wa Rhein-Main
(Elekezwa kutoka Uwanja wa ndege wa Frankfurt)
Kiwanja cha Ndege cha Rhein-Main ni kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Frankfurt am Main nchini Ujerumani. Ni kati ya nyanja za ndege kubwa ikiwa abiria zaidi ya milioni 55 wanaopita.
Jina kamili kwa Kiholanzi ni Flughafen Frankfurt am Main au kwa Kiingereza Frankfurt international Airport. Kifupi chake ni FRA.
Ni kituo kikuu cha Lufthansa.
Kiwanja cha ndege kipo kilomita 12 kusini ya Frankfurt na safari kwa treni kutoka mjini ni dakika 20.