Salamanda
Vyura sahihi | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Salamanda wa Maroko (Pleurodeles walti)
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Nusuoda 3:
|
Salamanda ni wanyama wa oda Caudata katika ngeli Amfibia wafananao na mijusi. Wanatofautiana na vyura kwa kuwa na mkia hata katika hatua ya mnyama mzima. Ngozi yao haina magamba na ni laini na nyevu, lakini ngozi ya spishi nyingi za familia Salamandridae ni kama mahameli au ina sugu. Rangi ya salamanda ni nyeusi, kijivu au kahawia kwa kawaida, lakini madume ya spishi nyingi hupata rangi kali wakati wa kuzaa. Spishi kadhaa zina sumu katika ngozi yao na hizi zina daima madoa au milia ya rangi kali ili kuonya wanyama mbuai. Takriban salamanda wote wanatokea nusudunia ya kaskazini, lakini spishi kadhaa zinatokea Amerika ya Kusini. Spishi nne zinatokea Afrika tu, huko kaskazini (Maroko, Aljeria na Tunisia).
Ndubwi
haririNdubwi au viluwiluwi wa salamanda wanafanana na hawa wa vyura lakini wale wa salamada ni wembamba zaidi na matamvua yao ni makubwa kwa kawaida kuliko yale ya ndubwi wa vyura. Kabla ya kutoka maji wanakuza miguu minne. Spishi nyingi za Plethodontidae (salamanda bila mapafu) hazina ndubwi lakini mayai hutagwa nchini kavu na salamanda wadogo, siyo ndubwi, hutoka.
Spishi za Afrika
hariri- Pleurodeles nebulosus, Salamanda wa Aljeria (Algerian ribbed newt)
- Pleurodeles poireti, Salamanda wa Poiret (Edough ribbed newt)
- Pleurodeles walti, Salamanda wa Maroko (Iberian ribbed newt)
- Salamandra algira, Salamanda Madoa (North African fire salamander)
Picha
hariri-
Salamanda wa Maroko
-
Kiluwiluwi wa salamanda wa Maroko
-
Salamanda madoa