Viambishi awali vya vipimo sanifu

Viambishi awali
vya vipimo sanifu vya kawaida
Jina Kifupi Zao mtiririko
Peta P 1.000.000.000.000.000
Tera T 1.000.000.000.000
Giga G 1.000.000.000
Mega M 1.000.000
Kilo k 1.000
Hekto h 100
Deka da 10
(Kipimo
asilia)
(--)
1
desi d 0.1
senti c 0.01
mili m 0.001
mikro μ 0.000.001
nano n 0.000.000.001
piko p 0.000.000.000.001
femto f 0.000.000.000.000.001

Viambishi awali vya vipimo sanifu vinaeleza viwango vya vipimo sanifu vya kimataifa kuwa uwingi au sehemu ya vipimo hivi.

Mfumo huu haujui sehemu kama nusu au robo bali unatumia hatua za kidesimali yaani hatua za sehemu au wingi wa kumi.

Kwa kawaida uwingi wa kipimo huandikwa kwa herufi kubwa kama vile T (tera..), G (giga..) na M (mega..). Kinyume sehemu za kipimo huandikwa kwa herufi ndogo kama vile d (desi..), c (senti) na m (mili..) huandikwa kwa herufi ndogo. Viambishi awali vya "k" (kilo..), h (hekto..) na da (deka..) havifuati kawaida hii kwa sababu zilikuwa kawaida kabla ya mapatano kuhusu mtindo huu.

Mifano ya kawaida iko katika matumizi ya sehemu za mita: sentimita (sehemu ya 100) na milimita (sehemu ya 1000), na pia kilomita. Kwa uwingi zaidi si kawaida kutaja "megamita" ambayo ingekuwa sawa na kilomita 1000.

Kwa kutaja uwezo wa komyuta au ukubwa wa data za dijitali viambishi awali za juu zimekuwa kawaida kwa kutaja idadi ya baiti: megabaiti, gigabaiti na terabaiti.

Marejeo hariri