Vicky Kamata
Vicky Paschal Kamata (alizaliwa Tanga (mji), 18 Septemba 1978) ni mwanamuziki na mwanasiasa Mtanzania mwanachama wa chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alichaguliwa kuwa mbunge wa viti maalum kwa miaka 2010 – 2020. [1] Akiwakilisha wanawake wa mkoa wa Geita.
Pamoja na kuwa mwanamuziki mkongwe amekua akisaidia Jamii kupitia taasisi yake inayoitwa Victoria Foundation Archived 11 Aprili 2022 at the Wayback Machine. akiwa ni muanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2011.
Akiwa kama mwanamuzikk alitamba na nyimbo mbalimbalk na moja kati ya vibao vyake ambavyo hutamba mpaka sasa katika vituo mbalimbali vya Redio na Luninga ni wimbo wa wanawake na maendeleo ambao mpaka mwaka 2021 ulitimiza miaka 20.
Wimbo huo umekua ukitumika sana katika hafla mbalimbali zinazohusu wanawake na kuendeleza mijadala mizito yenye kuwapa nguvu wanawake duniani kote kujitambua na kuzijua haki zao katika kutafuta kipato.
Wimbo huo pia umemletea tuzo nyingi.
Vibao vingine alivyotamba navyo ni kama vile Sikumbuki Kuku, Fitina, Moyo wa Mtu kichaka, Mapenzi na Shule, Zingatia maadili, Nimeolewa nk.
Marejeo.
hariri- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |