Vigano ni hadithi fupifupi zinazosimuliwa kwa lengo la kueleza makosa au maovu ya watu fulani ili kutoa maadili mema yanayofaa kwa wanajamii.

Msaidizi wa Maktaba akiwasimuliwa watoto hadithi

Masimulizi ya vigano mara nyingi hutumia methali kama msingi wake wa maadili. Methali hiyo ndiyo hujengewa masimulizi yanayolenga kumwonya mwanajamii anayetenda kinyume na maadili ya jamii yake.

Kwa kawaida vigano hujengwa juu ya tukio (kisa kimoja) moja ambalo hutumiwa kuelezea maisha halisi ya jamii husika.

Tazama piaEdit