Visa vya Esopo
Visa vya Esopo vinatokana na masimulizi ya Esopo, ambaye inaaminika kuwa alikuwa ni mtumwa wa Kiafrika aliyeishi kati ya mwaka 620 na 560 Kabla ya Kristo katika Ugiriki wa Zamani. Visa vyake hutumiwa kutoa mafunzo na kuburudisha. Visa hivi hutumiwa kwa wingi katika vitabu vya watoto na vikaragosi.
Historia ya Esopo haijulikani vyema. Inaaminiwa kuwa alikuwa ni mtumwa aliyeachiliwa huru na baadaye alikuja kuuliwa na Wadeliphi. Baadhi ya wanazuoni wanaamini kuwa hakuna mtu aliyewahi kuishi katika historia aliyeitwa Esopo.