Viti vya outdoor bean bags

Kiti cha outdoor bean bags ni kiti cha fahari na sanasana huwa kwa nje ya nyumba ambapo watu hukalia huku wakigana ngano na kuhadithiana kulingana na vile wameshinda kwa siku.

bean bags

Kiti hiki huwa kimetengenezwa na kitambaa laini na vitu vingine vyororo ambavyo hukifanya kiti hiki kiwe cha kufurahisha kwa starehe yake.

MatumiziEdit

Kiti cha outdoor bean bags chaweza kutumika kwa nje wakati watu wanakwenda kwa ziara au camp ya nje. Hata hivyo, yafaa uwe mwangalifu sana isije kwamba kiti kikatumika kunako hewa mbaya yenye mvua maana kiti hiki kitaharibika.

HistoriaEdit

Bean bag ya kwanza ilitengenezwa na Piero Gatti, Cesare Paolini na Franco Teodoro mwaka 1969 katika kampuni yao ya Zanota nchini Italia. Baadaye, outdoor bean bag zimekuwa kwa kila nyumba huku zikiuzwa kama fanicha kwa kutumia mtandao. Ujenzi wake pia umebadilika huku kampuni tofauti tofauti zikibuni njia mbalimbali za kuzitengeneza.

Ni nini haswa kinachotengeneza viti hivyoEdit

Bean bag za watoto za kuchezea hutengenezwa kwa kutumia maharagwe yaliyokaushwa. Pia huenda ukatengeneza kwa kutumia vijiwe vya PVC. Hata kama jina bean bags laashiria kwamba hutengenezwa kwa kutumia maharagwe, kuna vitu vingi vinavyoweza kutengeneza outdoor bean bags. Hizi ni kama:

  1. Ngozi
  2. Courdroy
  3. Fake fur
  4. Suede