Mbunge

(Elekezwa kutoka Wabunge)

Mbunge ni mwakilishi wa wananchi katika bunge.

Wabunge nchini Misri mwaka 1975

Katika nchi mbalimbali anawakilisha hasa wale wa jimbo kililomchagua.

Mara nyingi kuna wabunge wa kuchaguliwa na wale wa kuteuliwa.

Nchini Tanzania

hariri

Sehemu ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inasema: “Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa katiba hii”

Ibara ya 63(2), pia na Ibara ya 64(1) inaelezea kazi za Bunge, juu ya kutunga sheria.