Mwakilishi
Mwakilishi ni mtu anayemwakilisha mwingine mahali fulani au ni mtu anayefanya kitu kwa niaba ya mwingine. Hivyo basi mwakilishi anaweza kufanya kazi zile au zote ambazo zingefanywa na mtu anayemuwakilisha mahali husika na kwa wakati husika.
Wawakilishi wapo wa aina tofauti: kuna mwakilishi wa wilaya au jimbo, huyu hujulikana kama mbunge. Pia kuna mwakilishi wa kata fulani ambaye hujulikana kama diwani, lakini pia kuna mwakilishi wa nyumba kumi huyu hujulikana kama mjumbe.
Wawakilishi wa kampuni binafsi na serikali hujulikana kama mawakala.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwakilishi kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |