Wamata
WAMATA ni shirika lisilo la kiserikali katika Tanzania ambalo linajihusisha katika masuala yanayokabili watu walio na VVU na wanaoathiriwa na UKIMWI katika nchi hiyo.[1] Linaendesha kliniki ya ukimwi ya zamani kuliko zote katika Tanzania.[2] Jina lake linamaanisha "Walio Katika Mapambano Na AIDS Tanzania." WAMATA ilianzishwa mwezi wa saba 1989 na kundi dogo la wataalamu wa afya na familia kwa ajili ya kuwasaidia watu waishio na utambuzi wa VVU/UKIMWI.[3] Theresa Kaijage aliongoza shirika hilo akiwa mkuu wa kazi ya jamii na tiba ya familia katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili na pia alikuwa mhadhiri katika Taasisi ya Mafunzo ya Ustawi wa Jamii. Alitafuta fedha na msaada wa wajitoleaji, hatimaye akafanikiwa kupata ofisi ndogo katika Catholic Brothers of Christian Institution. Mahali hapo alianza kutoa ushauri na msaada kwa waathirika wa vvu/ukimwi.
WAMATA ilisajiliwa rasmi kama shirika lisilo la kiserikali tarehe 21 ya mwezi wa tatu, 1990. Mwaka 1992 tawi lingine liliasisiwa katika Rubya/Bukoba (magharibi ya Ziwa Nyanza) kuhudumia watu wa Mkoa wa Kagera. Lingine lilianzilishwa katika Mwanza mwaka huo huo. Matawi haya yanafanya shughuli peke yao.
WAMATA inAshirikiana na National AIDS Control Program (NACP).
Tanbihi
hariri- ↑ Iliffe, John (1998). East African Doctors: A History of the Modern Profession. Cambridge University Press. uk. 237. ISBN 0-521-63272-2.
{{cite book}}
: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help) - ↑ Reyes, Damaso. "Tanzanian AIDS Clinic Offers Frayed Lifeline". Retrieved on 2008-05-18. Archived from the original on 2007-08-21.
- ↑ OECD (1996). Development Co-operation Review Series. OECD Online Bookshop. uk. 57. ISBN 92-64-14821-3.
Viungo vya Nje
hariri- Official site Archived 5 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.