Mkoa wa Kagera kati ya mikoa 31 ya Tanzania ndio mkoa wa kaskazini-magharibi kabisa wenye postikodi namba 35000. Jina lake linatokana na mto Kagera.

Mkoa wa Kagera
Mahali paMkoa wa Kagera
Mahali paMkoa wa Kagera
Mahali pa Mkoa wa Kagera katika Tanzania
Majiranukta: 1°55′S 31°18′E / 1.917°S 31.300°E / -1.917; 31.300
Nchi Tanzania
Wilaya 8
Mji mkuu Bukoba
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Meja General Marco Gatitu
Eneo
 - Jumla 40,838 km²
 - Kavu 28,953 km² 
 - Maji 11,885 km² 
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 2,989,299
Tovuti:  http://www.kagera.go.tz/
Mandhari ya Kagera.

Mkoa wa Kagera umepakana na Burundi, Rwanda na Uganda upande wa Magharibi na Kaskazini. Upande wa Kusini umepakana na mikoa mingine ya Tanzania, yaani Kigoma, Shinyanga na Geita.

Eneo lake ni km² 28,953 za nchi kavu na km² 11,885 za maji ya ndani, hasa ya Viktoria Nyanza, jumla km² 40,838.

Mkoa wa Kagera uko mnamo mita 1000 juu ya uwiano wa bahari.

Makao makuu ya mkoa ni mji wa Bukoba.

Kiutawala eneo la mkoa limegawiwa kwa wilaya nane: Bukoba, Misenyi, Muleba, Karagwe, Ngara, Biharamulo na Kyerwa pamoja na manisipaa ya Bukoba. Misenyi ni wilaya mpya iliyoanzishwa mwaka 2007 na Kyerwa ikafuata mwaka 2012.

Sensa ya mwaka 2022 imeonyesha idadi ya wakazi kuwa 2,989,299 inayoendelea kuongezeka kasi [1].

Mkoa huu una makabila makubwa manne ambayo ni Wahaya, Wanyambo, Wahangaza na Wasubi. Wahaya huishi kwa wingi katika wilaya za Bukoba, Muleba na Misenyi, Wanyambo huishi kwa wingi katika wilaya za Kyerwa na Karagwe, Wahangaza huishi kwa wingi katika wilaya ya Ngara, na Wasubi huishi kwa wingi katika wilaya ya Biharamuro.

Makabila ya Wanyambo na Wahaya hupenda kula ndizi kwa wingi na asilimia kubwa wanafuata mila na desturi za mababu: zamani Wanyambo na Wahaya walikuwa hawawezi kuoana na hiyo bado sasa ipo kwa kiasi kidogo.

Pia mkoa huu una wakimbizi wengi, kwa asilimia kubwa wanatokea nchi za Rwanda na Burundi wakipitia wilaya ya Ngara.

Jiografia hariri

Hali ya hewa ni nzuri kwa kuishi, kilimo, uvuvi. Mkoa huo ni maarufu kwa ulimaji wa kahawa, ndizi, miwa na chai.

Pia una mbuga za wanyama na umezungukwa na mto Kagera.

Historia ya mkoa hariri

Mkoa huu unapatikana ukanda wa ziwa Viktoria. Katika mkoa huu kuna mambo mengi ambayo yalitetemesha nchi ya Tanzania. Mambo hayo ni pamoja na vita ya Uganda na Tanzania, vita ambavyo vilihusishwa na mkoa huu; ilikuwa mwaka 1978.

Ndipo Idd Amin Dada aliyekuwa Rais wa Uganda alipoliamru jeshi lake kuvamia mkoa wa Kagera. Walianza kuvamia wilaya ya Missenyi. Hapo Julius K. Nyerere aliyekuwa rais wa Tanzania aliamuru jeshi lake kufukuza wavamizi hadi kuvamia nchi ya Uganda.

Agizo hilo lilikuwa zuri lakini vijana wa mkoa wa Kagera walipata shida kwa sababu walilazimishwa kufuzwa Uanamgambo mara moja na kupelekwa vitani. Walipoanza tu vita hivyo raia wa Uganda walishirikiana na jeshi la Tanzania kufichua maficho ya jeshi la Uganda. Jeshi la Tanzania liliwapiga na kuwapora mali zao, vifaa vya kivita na kuwateka wanajeshi wao.

Mwanzoni mwa mwaka wa 1979 Idd Amin Dada alikimbia na Tanzania kushinda vita hivyo. Mara baada ya vita hivyo Watanzania walichukua mali za Uganda, hasa mifugo, na walipofika nchini Tanzania walifurahia na kusherekea ushindi huo.

Mwaka 1996 meli ya MV Bukoba ilizama ikisafirisha abiria kutoka mkoa wa Kagera kwenda Mwanza; watu wengi walikufa na lilikuwa pigo kwa serikali, kwa ndugu na majonzi makubwa kwa Watanzania kwa ujumla. meli hiyo ilikuwa ina mkoani mwanza katika ziwa la victoria

Katika mkoa huohuo mwaka 2016 lilitokea tetemeko la ardhi lililoleta maafa makubwa: watu walikufa, wengine walipoteza mali zao, hususani majumba yao. Uongozi wa mkoa wa Kagera uliomba kila Mtanzania kuchangia angalau shilingi 100 na kuwasaidia.

Elimu hariri

Katika mkoa huu elimu bado haijaenea kwa watu wote walioko vijijini. Elimu inakua kwa kasi ndogo na watu wengi wa mkoa huu hawajasoma: wengi wanafanya kazi ya kulima. Hali hiyo hufanya taifa kurudi nyuma kimaendeleo maana taifa kama taifa huongozwa na wasomi ili kukua kiuchumi.

Majimbo ya bunge hariri

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Kagera kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.