Wenzo ni mashine sahili inayosaidia kuhamisha na kupandisha mizigo mikubwa kwa kutumia nguvu ndogo.

Kwa wenzo mtu anapandisha mzigo mkubwa

Kimsingi ni pau kama gogo, mti au nondo inayowekwa chini ya mzigo kwa upande moja na kushikwa upande mwingine. Wenzo hulala juu sehemu ya mhimili inayoitwa "nukta fungwa" na nukta hii ni mahali pa kugeuza wenzo. Nukta fungwa inagawa wenzo kwa sehemu mbili zinazoitwa "mkono mzigo" na "mkono kani".

Utaratibu wa wenzo ni kimsingi ya kwamba kani ndogo kwenye mkono kani mrefu inapandisha mzigo mkubwa kwenye mkono mzigo mfupi.

Nguvu ya wenzo

hariri
 
Kanuni ya nguvu ya wenzo: kani upande wa mzigo F1; urefu wa mkono mzigo D1; Kani ya kuinulia F2; urefu wa mkono kani D2;

Kanuni ya nguvu ya mwenzo inasema:

„Kani zidisha urefu wa mkono kani ni sawa na mzigo zidisha urefu wa mkono mzigo"
(Kani ya kuinulia FK; urefu ni D; urefu wa mkono kani DK; kani upande wa mzigo FM; urefu wa mkono mzigo DM)
 
 
Kwa kutumia wenzo kani ndogo ya 5 kg inaweza kuwa sawa na kani ya 100 kg.

Utaalamu

hariri

Watu waligundua nguvu ya mwenzo tangu kale. Wamisri walitumia nyenzo waliposafirisha mawe makubwa kwa ujenzi wa piramidi.

Mtaalamu wa Ugiriki ya Kale Archimedes alikuwa mtu wa kwanza wa kuelewa na kutamka kanuni ya nguvu ya wenzo: "Uzani mbili sawa zikiwa na umbali sawa na nukta fungwa ziko katika hali ya msawazo, na uzani mbili sawa zisizo na umbali sawa hunama upande wa uzani ulio mbali zaidi".

Maarufu ni sentensi yake "Nipe wenzo ndefu ya kutosha na mahali imara pa kusimama nitahamisha dunia yote".


  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wenzo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.