Archimedes

Archimedes (287-212 KK) alikuwa mtaalamu wa Ugiriki ya Kale. Alikuwa mwanahisabati, mwanafizikia, mwanaastronomia na pia mvumbuzi wa vifaa mbalimbali vilivyokuwa vielelezo wa teknolojia iliyotumia matokeo ya sayansi.

Sanamu ya kisasa ya Archimedes.

MaishaEdit

Archimedes alizaliwa katika mji wa Siracusa kwenye kisiwa cha Sisilia (leo nchini Italia). Wakati ule miji ya Sisilia Mashariki iliundwa na kukaliwa na Wagiriki.

Baba yake Phidias alikuwa mwanaastronomia; kuna uwezekano alitoka katika ukoo wa mfalme wa mji.

Archimedes alipofikia umri wa miaka 10 alienda masomoni huko Aleksandria (Misri) iliyokuwa pia kitovu cha elimu ya Kigiriki pamoja na maktaba yake maarufu.

Hakuna habari zaidi juu ya maisha yake kama alioa au alikuwa na watoto.

Kazi zakeEdit

Archimedes ahesabiwa kati ya wataalamu muhimu zaidi katika historia ya hisabati na fizikia.

FizikiaEdit

 
Wenzo katika hali ya msawazo:
Kani upande wa mzigo F1; urefu wa mkono mzigo D1; Kani ya kuinulia F2; urefu wa mkono kani D2;

Nguvu ya wenzoEdit

Alikuwa mtu wa kwanza wa kuelewa na kutamka kanuni ya nguvu ya wenzo: "Uzani mbili sawa zikiwa na umbali sawa na nukta fungwa ziko katika hali ya msawazo, na uzani mbili sawa zisizo na umbali sawa hunama upande wa uzani ulio mbali zaidi".

Hapa aliweka msingi kwa sayansi ya umakanika. Maarufu ni sentensi yake "Nipe wenzo ndefu ya kutosha na mahali imara pa kusimama nitahamisha dunia yote".

Kanuni ya ueleajiEdit

Vilevile aligundua kanuni ya ueleaji inayoitwa pia "kanuni ya Archimedes" kuwa "gimba linalowekwa katika kiowevu linasukumwa juu kwa nguvu iliyo sawa na uzito wa kiowevu kinachosogezwa kando na gimba hili". Alingundua kanuni hii alipopewa kazi ya kufanya utafiti kama taji la mfalme wa Siracusa lilikuwa dhahabu tupu au kama dhahabu ilizimuliwa kwa kuchanganya na fedha. Hapa kuna hadithi ya kwamba aliona usuluhisho siku moja alipooga bafuni akiona jinsi maji yalivyopanda juu alipoingia ndani yake. Hapa Archimedes alielewa ya kwamba aliweza kupata mjao wa taji kwa kuizamisha katika maji. Kwa kupima mjao na uzito aliweza kugundua kama taji lilikuwa dhahabu tupu au la kwa sababu aliweza kulinganisha kiasi cha mjao wa dhahabu tupu chenye uzito uleule.

 
Skrubu ya Archimedes
 
Skrubu ya Archimedes ya kisasa huko Uholanzi

Kuna taarifa ya kwamba baada ya kushika hoja hii bafuni aliita kwa sauti kubwa "Heureka!" (Kigiriki "εύρηκα!" - nimeigundua!) akatoka mara moja katika bafu na kukimbia barabarani uchi.

MitamboEdit

Archimedes hakuwa mwanasayansi pekee lakini alitengeneza pia mitambo mbalimbali alipotumia nadharia zake.

Skrubu ya ArchimedesEdit

Kwa kazi ya kutoa maji katika meli aligundua aina ya skrubu ya kusukuma maji juu. Skrubu hii ilizungushwa ndani ya bomba. Machine imeendelea kutumiwa hadi leo hasa kwa umwagiliaji pale ambako ni lazima kusukuma maji kutoka uwiano wa chini kwenda juu.

SilahaEdit

Archimedes alitengeneza na kuboresha silaha mbalimbali zilizotumiwa katika vita ya 214-212 KK wakati Waroma walishambulia mji wa Siracusa.

Kati ya vifaa alivyotengeneza vilikuwa:

  • vioo vya parabola vilivyokusanya nuru ya jua na kuwasha moto manowari za Waroma
  • winchi kubwa zilizoweza kushika kuinua na kuangusha manowari za Waroma zilipokaribia ukuta wa bandari ya Siracusa
  • katapulti au pinde kubwa za kufyatulia mawe au mishale mikubwa dhidi ya manowari

Kifo cha ArchimedesEdit

Hata hivyo Waroma walifaulu kuvuka kuta za mji na kuingia Siracusa. Wakati ule Archimedes alikuwa kwake nyumbani akitafakari kanuni za hisabati kwa kuchora duara katika mchanga. Wanajeshi Waroma walipoingia nyumbani mwake Archimedes aliita "Msivuruge duara zangu!" na Mroma aliyekasirika alimwua.

KumbukumbuEdit

Kwa heshima ya Archimedes mahali pafuatapo paliitwa kwa jina lake: