Wiki ya Uhuru wa Maoni
Wiki ya Uhuru wa Maoni (kwa Kiingereza: Free Speech Week; inajulikana pia kama "Wiki ya Kitaifa ya Uhuru wa Maoni") ni adhimisho la kitaifa la uhuru wa maoni na wa kujieleza katika nchi ya Marekani. Wiki hiyo huadhimishwa muda wote wa wiki ya tatu ya mwezi Oktoba kila mwaka.
Kulingana na waandaaji, malengo ya wiki ya uhuru wa maoni ni kuifanya jamii kujiamini na kuona umuhimu wa wiki na uhuru wa maoni kidemokrasia na kusherehekea uhuru."[1]
Dhana
haririUhuru wa maoni ni wiki inayotoa nafasi kwa mtu mmojammoja na asasi mbalimbali katika kutengeneza mahusiano bora na kuona umuhimu wa kujitolea. Sherehe hizo huandaliwa ili kuwajengea watu mazoea na tabia ya kujiamini katika kutoa maoni yao kwa uwazi na kujielezea wao wenyewe na kuongeza mahusiano katika uhuru huo.
Historia
haririShirika lisilo la kifaida la "Media Institute", linalopatikana Arlington, Virginia, lilianzisha wazo la wiki ya uhuru wa maoni mwaka 2003. Wazo likiwa ni katika kukuza mpango wa "Cornerstone Project", mpango wa kwanza wa mabadiliko ulikamilika mwaka 2003.
Mwaka 2005, waliiomba taasisi ya "National Association of Broadcasters Education Foundation" (NABEF) kuungana pamoja ili kuikamilisha wiki hiyo. Baadaye asasi nyingine mbili zikaomba pia kuungana katika kuikamilisha wiki hiyo ya uhuru wa maoni .”[2]
Mwaka 2005 walisherehekea miaka mitano ya kuungana na kufanya kazi pamoja kama asasi tano ambazo ni "American Association of Advertising Agencies", "American Bar Association", "Americans for the Arts", [["National Constitution Center" katika jiji la Philadelphia, na "National Endowment for the Humanities".
Tangu mwaka 2005 asasi hizo zimekuwa zikishirikiana na kampuni za habari na makampuni mengine kama magazeti katika kuitangaza wiki hiyo, vyuo vingine vya sheria vimekuwa pia vikishirikiana nao katika kuitimiza siku hii.
Mwaka 2011 jina lilifupishwa na kuwa "Wiki ya Maoni Huru".”[3] Asasi nyingine zilitengeneza mabaraza ya kishauri mwaka 2012 ili kuitiliza nguvu zaidi wiki hiyo. Tarehe 30 Julai 2012, Robert Pittman, mkurugenzi wa "Clear Channel" na "Communications Inc"., alitangaza kukubali kuwa mwenyekiti wa baraza la ushauri la wiki ya uhuru wa maoni.[4][5]
Mawazo na Siasa
haririWiki ya Uhuru wa Maoni inaweza kuwa ni tukio la kisiasa na pia jukwaa la mawazo huru kulingana na waandaaji wa wiki ya uhuru wa maoni ilikuwa ni kuunganisha na kuthaminisha uhuru wa maoni.”[6]
Tazama Pia
haririViungo vya Nje
hariri- Free Speech Week (www.freespeechweek.org)
- The Media Institute (www.mediainstitute.org)
Marejeo
hariri- ↑ "Overview of Free Speech Week." Overview of Free Speech Week. The Media Institute, n.d. Web. 24 Sept. 2012. <http://www.freespeechweek.org/?p=652>.
- ↑ Wharton, Dennis. "NAB Education Foundation and The Media Institute Announce Inaugural 'Freedom of Speech Week'" NAB News Release:. National Association of Broadcasters, 3 Oct. 2005. Web. 24 Sept. 2012. <http://www.nab.org/documents/newsroom/pressRelease.asp?id=1151>.
- ↑ Eggerton, John. "The Media Institute Launches Free Speech Week." Broadcasting & Cable, 17 Oct. 2011. Web. 12 Oct. 2012. <http://www.broadcastingcable.com/article/475352-The_Media_Institute_Launches_Free_Speech_Week.php>.
- ↑ Kaplar, Richard. "Clear Channel CEO Bob Pittman To Head New Free Speech Week Advisory Council." The Media Institute. The Media Institute, 30 July 2012. Web. 24 Sept. 2012. <http://www.mediainstitute.org/PressReleases/2012/073012.php Ilihifadhiwa 23 Machi 2017 kwenye Wayback Machine.>.
- ↑ Eggerton, John. "Pittman To Promote Media Institute's Free Speech Week." Cable Television News. NewBay Media, LLC, 30 July 2012. Web. 12 Oct. 2012. <http://www.multichannel.com/node/18147>.
- ↑ "Overview of Free Speech Week." Overview of Free Speech Week. The Media Institute, n.d. Web. 24 Sept. 2012. <http://www.freespeechweek.org/?p=652>.