Wikipedia:Jamii
Uhamasishaji/Utangazaji
haririMalengo:
- Kutengeneza kamusi elezo kubwa ya Kiswahili itakayotumiwa na mtu yeyote bila gharama
- Kutafuta matumizi ya kamusi elezo hii mashuleni na kwenye miradi mbalimbali ya kielimu; kutumia yaliyomo ndani ya kamusi elezo hii (ambayo inapatikana kwa lugha mbalimbali)kwa faida za wazungumzaji wa Kiswahili na wale wanaojifunza Kiswahili
- Kushirikiana na wanafunzi wa vyuo vikuu na walimu wa lugha kuchangia na kuendeleza matumizi na mchango wa kazi hii
Kinachotakiwa:
- Orodha ya watu watakaojitolea,
- Orodha ya wanafunzi wenye hamu ya kushiriki,
- Orodha ya walimu wenye nia ya kushiriki na programu muafaka za kielimu
- makala fupi za msingi za maarifa duniani
Watu wenye nia ya kushiriki
hariri- Sultanseifu (Tanzania)
- Ndesanjo
- Sj (Boston)
- Jeff (Toronto)
- Mshairi (Uingereza)
- Richard Mabala (Ethiopia/Tanzania)
- Joseph Tungaraza(Oz)
- Makene (Texas)
- Stan
- Herry Ibrahim (Tanzania) (Revolución) kutoka Florida
- maitha (kenya)
- Zablon Mgonja(Mtanzania) Chuo kikuu cha FISK marekani
- Matt Crypto (UK)
Walimu na wanafunzi
- Chuo Kikuu cha Nairobi
- Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam
- Shule za sekondari
- Kwingineko wanakofundisha lugha
Wanablogu wa Kiswahili na wataalamu wa teknolojia ya kompyuta
- Wanablogu wa Kenya naTanzania
- Uhamasishaji wa mdomo kupitia watu mbalimbali kama Ory, Ndesanjo, Jeff, Joseph, Nkya, Maitha, n.k.
Mambo ya awali ya kuweka kwenye kamusi elezo
haririOrodha ndefu: makala fupi za msingi za maarifa duniani; tuanze na makala 1000.
- Makala zilizoko kwenye kamusi elezo za Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, n.k. zinaweza kusaidia wanaoshiriki kuandika makala za awali za Kiswahili
Orodha fupi:
- Orodha ya Waafrika mashuhuri
- Wanasiasa: Wanasiasa wa mataifa ya Afrika
- Wasanii na waaandishi wa vitabu:
Mapendekezo ya mambo mengine ya kujumuisha katika kamusi elezo hii yanakaribishwa.
Mikutano ijayo
haririKawaida mikutano hufanyika kupitia teknolojia ya IRC
Mkutano wa mwisho ulipangwa kufanyika jumamosi ya tarehe kwanza, Oktoba, 2005.
Malengo ya kutimiza kabla ya mkutano ujao:
#1: kuongeza idadi ya washiriki katika mkutano ujao #2: kuongeza idadi ya watu watakaoshiriki kuhariri kamusi elezo hii #3: kutafsriri ukurasa wa wikipedia:jamii #4: kuweka viunganishi vya makala au mambo yanayohusiana ndani ya makala mbalimbali za Kiswahili
Maoni
haririTafadhali weka maoni na mawazo yako katika ukurasa wa mazungumzo. Sj