Wikipedia:Kiswahili Wikipedia Challenge/Ruth Wambua - Mutua

Mtoto humtunzavyo ndivyo akuavyo.

Maana ya nje ya msemo huu ni kusema ya kwamba mambo unayomfunza mtoto akiwa mchanga, ndiyo huendelea kuyajua. Hatimaye, mtoto huyu hubakia kujua na kufuata mambo aliyoyazoea. hivi ni kuumaanisha ya kwamba alichozoea ndicho atakachoendelea kufanya. Kwa mfano, ikiwa mtoto amezoea kutowaheshimu wakubwa wake, hata akikua ataendelea vivyo hivyo. Vile vile, kama mtoto amezoea kuwatendea mema watu wengine, hivyo hivyo ndivyo ataendelea kufanya hata akikomaa.

Maana ya ndani ya msemo huu ni kwamba, mambo ambayo mtu anayoyazoea akiwa mdogo, huwa ni vigumu kuyasahau anapokomaa. Msemo huu utumika kuwasuta wazazi ambao wana tabia ya kutowakosoa watoto wao wanapokosa au kufanya mambo yasiyostahili. kwa mfano, mkubwa wako anapokusalimia, ni tabia nzuri kumjibu. Vili vile, ni vyema kuwaheshimu wakubwa wako kwa vyovyote vile.


--ruthdeshy 09:18, 1 Desemba 2009 (UTC)

KWC Mtumiaji huyu ni mshiriki katika Shindano la Wikipedia ya Kiswahili la 2009.   (Submissions)
(for individuals)  Own work.  own transalation.