Wikipedia:Makala ya wiki/Tangazo kuhusu utaratibu mpya kwa majina ya akaunti

Nembo ya Wikimedia

Tangazo

Kuanzia Mei 27 2013 tutaona mabadailiko katika utaratibu wa majina ya akaunti za watumiaji waliojiandikisha.

Wengi wetu wamejiandikisha katika Wikipedia ya Kiswahili ambayo ni wiki mmoja kati ya wiki 900 chini ya Wikimedia. Lakini wengine wana pia akaunti kwenye English Wikipedia, Commons, na kadhalika. Hadi sasa tuliweza kuchagua jina la akaunti jinsi tulivyopenda; yaani kama jina halikuchukuliwa na mwingine tayari tuliweza kulichagua.

Kwa hiyo iliwezakana ya kwamba watumiaji mbalimbali waliweza kuchagua jina lilelile kwenye wiki tofauti bila kujua. Yaani imewezekana Sam wa sw.wikipedia alikuwa mtu tofauti na Sam wa en.wikipedia au Sam wa de.wiktionary. Kutokana na ushirikiano wa karibu zaidi kati ya aina za wiki hali hii ilisababisha usumbufu na kazi nyingi.

Kuanzia 27 Mei kutakuwa na kila jina mara moja tu na hii kwa wiki zote za Wikimedia. Kuanzia sasa kama mtu yeyote anafungua akaunti mpya na kuchagua jina atapimwa na orodha ya Wikimedia yote itakayomrihusu kuchagua jina Fulani kama hili halikuchukuliwa bado na mt mwingine katika wiki yoyote chini ya Wikimedia.

Lakini wale wenye majina yanayopatikana pia katika wiki nyingine wataona usumbufu kidogo wakitafakari kubadilisha majina yao.

Kwa mfano kama hao akina Sam wa mfano wa juu wataona majina yao kubadilishwa kuwa

  1. a) Sam~ sw.wikipedia
  2. b) Sam~ en.wikipedia
  3. c) Sam~ de.wiktionary

maana haitawezekana tena kutumia jina lilelile kwa watu tofauti wenye wiki tofauti.

Programu itaendelea kutambua michango yako yote ya awali na kila mtu anayerejea mchango wako atakutambua.

Ila tu kama unaathiriwa na mabadiliko haya na hupendi kuendelea na hili jina refu – basi kila mmoja aende hapa Meta na kutafuta jina jipya. Hata hili jina mpya iunganishwa na mchango yote ya awali. ►Soma zaidi