Wikipedia:Makala ya wiki
Maelezo
Ukitaka kupeleka makala hapa (itaonekana baadaye kwenye ukurasa wa Mwanzo kwa kubadilishana na nyingine)
- A) Chagua makala unaotaka kuonyesha kwenye ukurasa wa kwanza
- B) tunga hitimisho fupi ya makala hii (si zaidi ya alama 1100) na kuihifadhi kwa jina la Wikipedia:Makala ya wiki/XXXXXXX - badala ya XXXXXXX andika jina la makala
- Andika jina la makala uliyotunga hapa badala ya jina la nyingine. Usiongeze idadi kwa jumla!
- katika makala hii kopi Kigezo:Makala ya wiki
- |jina= (jina la makala) Badala ya mabano andika jina la makala.
- |picha= (jina la picha) Badala ya mabano andika jina la faili ya picha.
- |nakala ya picha = (matini itakayoonekana chini ya picha) Badala ya mabano andika maelezo ya picha.
- |makala = (sehemu ya makala uliyochagua - izizidi alama 1100 - 1150) Badala ya mabano andika sehemu ya makala uliyochagua - izizidi alama 1100. Tofauti na kawaida weka maneno ya kwanza yenye jina la makala kwa mabano mraba mfano [[Wolfgang Amadeus Mozart]] maanake hii inasidia kufungua makala yenyewe.
Mwisho wa maelezo - hariri chini yake
Kassim Said Mapili (1937 - 2016) alikuwa mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi kutoka nchini Tanzania. Mzee Mapili alizaliwa katika kijiji cha Lipuyu, Tarafa ya Lionya, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi mwaka 1937. Hivyo umauti umekuta Mzee Mapili akiwa na umri wa miaka 79. Alipata elimu ya msingi huko kwao Lipuyu, sambamba na kupata elimu ya dini na mwenyewe aliwahi kusema alianza kupata mapenzi ya kuimba wakati alipokuwa Madrasa akighani Kaswida. Mwaka 1958 alijiunga na White Jazz Band iliyokuwa na masikani yake huko Lindi.
Mwaka mmoja baadaye akahamia Mtwara na kujiunga na Mtwara Jazz Band, lakini mwaka 1962 akajiunga na Honolulu Jazz Band ambayo nayo ilikuwa hapo hapo Mtwara. Mwaka 1963, Mzee Mapili akachukuliwa na TANU Youth League ya mjini Lindi, na kujiunga na bendi ya Jamhuri Jazz Band ya hapo Lindi. Mwaka 1964 Mzee Mapili akachaguliwa kuanzisha bendi ya TANU Youth League ya Tunduru. Mwaka mmoja baadaye alihamia Kilwa Masoko na kujiunga na Lucky Star Jazz Band ya mji huo. ►Soma zaidi