Wikipedia:Mwongozo (Kujisajili)
Utangulizi | Kuhariri | Kuanzisha Makala | Muundo | Viungo vya Wikipedia | Kutaja vyanzo | Kurasa za majadiliano | Kumbuka | Kujisajili |
Kujisajili kama mtumiaji
Kila mtu anaweza kuchangia kwenye Wikipedia hata bila kujiandikisha.
1. Faida za kujisajili
Kujisajili kunaleta nafasi za nyongeza na faida hasa ukichangia mara kwa mara. Hasa:
- unapata nafasi zaidi za kuhariri, kwa mfano kama ukurasa umehifadhiwa
- unapata ukurasa wa "Maangalizi yangu" unaosaidia kutazama makala unazopenda kufuatilia.
- unaweza kuhamisha kurasa (lakini kumbuka sheria zake)
- ni rahisi kutambuliwa na kuheshimiwa na wengine kwa sababu wanakujua kutokana na michango yako
- wengine wanaweza kuwasiliana nawe kwenye ukurasa wako wa majaidiliano
2. Kufungua akaunti
- Hatua ya kwanza ni kubofya kwenye kona ya juu na baadaye tena kwa "kujisajili".
- Kwa usalama wa Wikipedia ni lazima kutaipu herufi zinazoonyeshwa katika dirisha dogo chini yake.
- Sasa unaingiza jina ulivyojichagulia na nywila (neno lako la siri) mara mbili.
- anwani ya baruapepe si lazima; lakini unashauriwa kuiandikisha! Inasaidia kama unapenda kuwasiliana na watumiaji wengine kwa njia hiyo. Unaweza pia kuiacha kwanza na kuiongeza baadaye.
- Mwishoni unabofya chini "sajili akaunti"
- Kama jina ulilochagua limeshachukuliwa na mwingine au kama umekosea kutaipu neno la siri mara mbili unaona dirisha unapaswa kuanza upya.
3. Kuingia
- Ukiwa mwenye akaunti na jina la Wikipedia unaweza kuingia kila safari unapofungua Wikipedia.
- Unabofya tena kwenye kona ya juu utapata dirisha la "Ingia".
- Sasa unaona viungo vipya kwenye mstari wa juu kabisa kama vile
- Jina lako - inafungua ukurasa wako binafsi
- Majadiliano yangu - inafungua majadiliano kwenye ukurasa wako
- Mapendekezo yangu - hapa unaweza kubadilisha kuonekana kwa kurasa zako
- Maangalizi yangu - inaonyesha orodha ya makala uliyochagua kufuatilia mabadiliko yao
- Michango yangu - inakupa orodha ya michango yote uliyofanya kwenye Wikipedia
- Toka - ukipenda kutoka kwa safari hii - baada ya kubofya hutakuwepo tena kwa jina hadi kuingia tena
- Kama mwandishi aliyejiandikisha utaonekana kwa watumiaji wote wengine - kwa mfano hivyo: Bofya hapa na andika jina la mtumiaji
4. Kuwezesha baruapepe
- Hakikisha kwamba umeingiza anwani yako ya baruapepe
- Bofya menyu "Mapendekezo" ("preferences")
- Tafuta chini "Hitiari za barua pepe"
- Bofya "Yakinisha anwani yako ya barua pepe"
- Sasa fungua baruapepe zako, utaona ujumbe kutoka Wikipedia / Wikimedia.org
- Thibitisha kwa kubofya "Confirm email address"
- Sasa kila mtumiaji aliyejiandikisha ataona menyu "Email this user" kwenye ukurasa wako. Anaweza kukuandikia lakini haoni anwani yako.