Wikipedia:Uharabu
Uharabu (kwa Kiingereza: vandalism) ni kuharibu makala za wikipedia kwa makusudi kwa kuongeza habari za uwongo au kuondoa habari sahihi. Msimamo na uadilifu wa Wikipedia unahatarishwa na matendo ya aina hii.
Uharabu ni tofauti na mabadiliko yanayoingiza makosa lakini hayaonyeshi nia mbaya.
Nia mbaya inaonekana kama:
- matini yote au sehemu kubwa ya matini ya makala ikifutwa tu na makala kuhifadhiwa baadaye bila matini au kubaki na sehemu chache, tena bila maelezo kwenye ukurasa wa majadiliano kutoa sababu
- kama makala inabadilishwa kwa kuingiza kashfa na matusi
- kuingiza picha zisizo na uhusiano wowote na mada au kulenga kukashifu (kama kuingiza picha za wanyama katika makala kuhusu mtu)
- kuingiza habari bila ukweli kama mzaha au kichekesho (sisi sote tunapenda mzaha mzuri, lakini ikibaki kwenye wikipedia inaunda habari ya uwongo ya kudumu, kwa hiyo hatucheki hapa!)
Ukijaribu uharabu kwenye wikipedia kubwa kama en.wiki inawezekana utaonywa tu. Hapa kwenye Wikipedia ya Kiswahili utafukuzwa haraka sana. Maana tuko waratibu wachache mno, kwa hiyo tunapendelea kumzuia mtu mara moja kwa wiki, miezi au milele ukionekana unaleta uharabu kwa makusudi.
Kama umebanwa lakini una sababu za kujitetea basi, lete hoja katika ukurasa wa jumuiya au katika ukurasa wa mkabidhi fulani.
Uharabu ukigunduliwa ufutwe.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |