Open main menu

Wikipedia β

Wikipedia

kamusi elezo huru mtandaoni

Wikipedia ni kamusi elezo huru ya lugha nyingi katika mtandao wa wavuti.

Inatumia taratibu za wikiwiki. Ni bure kabisa, na inaweza kusomwa, kuandikwa, na kuhaririwa na mtu yeyote, popote pale. Yaani kila mtu anaweza kuchangia makala akiwa na uhuru wa kuboresha makala zilizopo kwa kuzihariri.

Kamusi hii inajengwa kwa utaratibu huria ambao unategemea falsafa ya ushirikiano inayokuwa kwa kasi.

Falsafa hii inaonekana katika vuguvugu la programu huria ya tarakilishi, mikutano huria, demokrasia huria, n.k.

Wikipedia inaweza kusomwa pia nje ya mtandao kwa kutumia programu huria ya Kiwix.

Historia

Wikipedia ilianzishwa kwa Kiingereza mwezi Januari mwaka 2001.

Mwaka 2003 kamusi elezo hii ilianzishwa katika lugha ya Kiswahili.

Tazama pia

  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wikipedia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.