Wikipedia ya Kiingereza Rahisi
Wikipedia ya Kiingereza Rahisi au Simple English Wikipedia ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia ambalo limeandikwa kwa Kiingereza Rahisi.
Ilianza mwaka wa 2004. Mnamo Machi 2016, Wikipedia kwa Kiingereza Rahisi ina makala zipatazo 118,000. Makala nyingi za Simple ni fupi kuliko zile za Wikipedia kwa Kiingereza.
Kamusi elezo hiyo ilitakiwa itumike kwa ajili ya watoto, ambao huenda wasiwe na uwezo kuelewa vyema makala za Wikipedia ya Kiingereza, na watu wengine ambao bado wanajifunza Kiingereza.
Wahariri
hariri- Tazama orodha ya wahariri wa Simple.
Hii ni sawa tu na Wikipedia nyingine, ambazo zote makala zake huandikwa na watu wa kujitolea, pia kila mtu ana uwezo wa kubadili, kusahihisha na kutohoa maneno ya kamusi elezo ya Wiki.
Kuna baadhi ya wahariri ambao wana uwezo wa kufanya zaidi kwenye Wikipedia. Wanaitwa wakabidhi au wasimamizi na mabureaucrat au warasimu. Wao wana mamlaka ya kufuta makala, kuzihamisha, na kuzuia watu kuzibadilisha. Mabureaucrat wana uwezo pia wa kuwafanya watu wengine kuwa wakabidhi/wasimamizi.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wikipedia ya Kiingereza Rahisi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |