Wilaya ya Karonga
Wilaya ya Karonga ni wilaya mojawapo katika Kanda ya Kaskazini ya Malawi. Wilaya ina eneo la km² 3,355. Idadi ya wakazi ni 365,028. [1]
Ni wilaya ya mpakani kati ya Malawi na Tanzania, inayokaliwa zaidi na Wankhonde na matawi mengine ya Wanyakyusa.
Barabara kuu kutoka Tanzania hadi Malawi inapita mpaka katika kazkazini ya wilaya, kwenye kituo cha Songwe.
Makao makuu ya wilaya yapo Karonga mjini.
Uchumi
haririKatika miaka michache iliyopita, kumekuwa na maendeleo mengi katika wilaya hii kutokana na ugunduzi wa urani katika mgodi wa Kayelekera, uliofunguliwa rasmi mwaka 2009. Barabara nyingi za awali zilizokuwa na changarawe zimewekwa lami.
Utalii
haririKuna hoteli nyingi na nyumba za wageni huko Karonga, kando ya Ziwa Nyasa (inayoitwa hapa Ziwa Malawi) .
Mgawanyiko wa serikali na utawala
haririKuna majimbo bunge matano wilayani:
- Karonga - Kati
- Karonga - Kaskazini
- Karonga - Kaskazini Magharibi
- Karonga - Nyungwe
- Karonga - Kusini
Tangu uchaguzi wa 2009 Karonga Nyungwe imewakilishwa na mwanasiasa wa AFORD, na viti vingine vinashikiliwa na wanachama wa Democratic Progressive Party . [2]
Marejeo
hariri- ↑ "2018 Population and Housing Census Main Report" (PDF). Malawi National Statistical Office. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-06-08. Iliwekwa mnamo 25 Desemba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Parliament of Malawi - Members of Parliament - Karonga District". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-17. Iliwekwa mnamo 2011-01-19.