William "Bill" Kim

William "Bill" Kim ni jina la kutaja uhusika wa kipindi cha televisheni Kimarekani, maarufu kama Prison Break. Uhusika huu ulichezwa na Reggie Lee. Uhusika ulianza kuonekana ukiwa kama Ofisa wa Huduma za Siri, aliyeingia makataba na Rais Caroline Reynolds. Hata hivyo, baadaye iligundulika kuwa ni mwajriwa mwenye cheo kikubwa kabisa na "The Company".

Uhusika wa Prison Break

William Kim
Mwonekano wa kwanza: [[(sehemu ya Prison Break)|]]
Mwonekano wa mwisho: Sona
Msimu: 2
Imechezwa na: Reggie Lee
Pia anajulikana kama: bill kim
Kazi yake: Kachero wa Huduma ya Siri wa The Company

Kim alikuwa kiongozi mkubwa kabisa wa kuhondosha na kutoa vitisho kwa watu wa the Company, kwa mfano alipotoa mkwara mzito kwa hawa Fox River Eight na Aldo Burrows na mtandao mzima unaomfuata. Anaonekana kuwa anakosea kila kitu kwa kuwa na pupa mno.

Anajifanya kama yeye ni mtu wa kati wa Rais na Paul Kellerman (Paul Adelstein), kitendo ambacho kilisababisha mshikemshike katia yao. Mda mfupi baada ya Fox River Eight kutoroka, Kim akawa msimamizi mpya wa Kellerman.

Kellerman akaingiliwa na hofu kwa hili, akiwa kama yeye alikuwa akiripoti kazi zake kwa Reynolds moja kwa moja kwa takribn miaka 15. Kim alimwelezea Kellerman kwamba, hili linasababishwa na Reynolds kuwa na kazi nyingi za mambo mengine ya kufanya, ikiwa sambamba kabisa na mpango mzima wa kuondoa mambo mabaya aliyoyafanya.

Viungo vya Nje

hariri