Wingu la mashahidi

URL wingulamashahidi.org
Alexa Rank 135,000 (April 2020)

Wingu la Mashahidi ni tovuti ya Kikristo nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki.

Tovuti hii imeanzishwa mwaka 2018 kwa lengo la kufikisha habari njema za Yesu Kristo kwa watu waliopo Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki, pia kutangaza habari za ujio wa Pili wa Yesu, ambao umo karibuni kutokea.

Tovuti hii ilianza kuchapisha masomo yake kwa lugha ya Kiswahili mwaka 2018, lakini mpaka kufikia mwaka 2019 mwishoni iliongeza kuchapisha masomo hayo kwa lugha nyingine mbili ambazo ni Kiarabu na Kiingereza.

Tovuti ya Wingu la Mashahidi imekuwa inapokea watembeleaji zaidi ya elfu moja kwa siku. Kurasa zaidi ya elfu sita zinasomwa kwa siku.

Tovuti hii si ya kutengeneza pesa, wala hairuhusu matangazo yoyote ya kuiingizia fedha, wala haihimizi michango yoyote kutoka kwa wasomaji wake, isipokuwa ya wale wanaoguswa kwa hiari yao wenyewe kufanya hivyo.