Afrika ya Mashariki

Muhtasari wa masuala ya mazingira kusini mwa Afrika
(Elekezwa kutoka Afrika Mashariki)

Afrika ya Mashariki ni sehemu ya bara la Afrika ambayo iko upande wa mashariki, ikipakana na Bahari ya Kihindi.

Ramani ya Afrika Mashariki kadiri ya Umoja wa Mataifa.

Kadiri ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Mashariki ina nchi 18 zifuatazo:

  • Mayotte na Réunion, zilizokuwa makoloni na sasa ni mikoa ya Ufaransa, zinahesabiwa pia katika orodha hii.

Hata hivyo:

Historia

Afrika ya Mashariki inatajwa na sayansi kuwa mahali ambako watu wa kwanza duniani walikopatikana.

Majina ya miji ya Afrika ya Mashariki imetajwa mara ya kwanza katika Periplus ya Bahari ya Eritrea (karne ya 1 B.K.).

Tangu uenezaji wa ukoloni wa Kizungu upande wa Mashariki wa bara ulianza kuitwa Afrika ya Mashariki. Somalia, Eritrea na Ethiopia za leo zilitawaliwa na Italia kama "Afrika ya Mashariki ya Kiitalia" (Africa Orientale Italiana) katika miaka ya 1936 hadi 1941, Kenya ilitwaliwa na Uingereza kwa jina la "Afrika ya Mashariki ya Kiingereza" (East Africa Protectorate au pia British East Africa) hadi 1920, Tanganyika pamoja na Rwanda na Burundi zilijulikana kama "Afrika ya Mashariki ya Kijerumani" (Deutsch Ostafrika) hadi 1919 na Msumbiji iliitwa mara nyingi "Afrika ya Mashariki ya Kireno" (África Oriental Portuguesa) hadi uhuru.

Lugha

Wakazi wengi wa Afrika ya Mashariki ni wasemaji wa lugha za Kibantu; sehemu ya kaskazini wasemaji wa lugha za Kihamiti ni wengi (Waoromo, Wasomalia). Katika Ethiopia kuna wasemaji wengi wa lugha za Kisemiti. Pia kuna wasemaji wa lugha za Kiniloti na lugha za Khoisan.

Ushirikiano wa nchi za Afrika ya Mashariki

 
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Nchi mashuhuri zaidi katika sehemu hii ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi kwa sababu ya kutumia lugha moja katika mawasiliano baina ya wananchi wa sehemu hii, yaani Kiswahili.

Aghalabu nchi za Afrika ya Mashariki zinazungumza lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano kati yao, kwani katika nchi hizi kuna makabila mengi sana na kila kabila lina lugha yake ambayo kawaida inatumika nyumbani baina ya watu wa kabila moja, lakini wakitaka kuwasiliana na makabila mengine, mara nyingi hutumia lugha ya Kiswahili, na hii ni kwa sababu lugha hii ndiyo iliyoenea zaidi na kufahamika zaidi katika eneo hili la dunia.

Nchi za Afrika ya Mashariki, hasa Kenya, Uganda na Tanzania ni nchi ambazo ni karibu tangu zamani. Zimeshirikiana historia, zote zimekaliwa hasa na makabila yanayotumia lugha za Kibantu (Kenya na Uganda wana pia idadi muhimu ya wakazi wasiotumia lugha za Wabantu). Katika nchi zote tatu lugha ya Kiswahili imekuwa lugha muhimu ingawa kwa daraja mbalimbali. Wakati wa ukoloni zilitawaliwa na Uingereza iliyoacha taasisi na taratibu mbalimbali zilizosaidia kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakati wa uhuru.

Tanzania, Kenya na Uganda zina ukubwa wa eneo la maili za mraba; Tanzania 360,000 ikifuatiwa na Kenya 224,960 na Uganda 93,980 upande wa mashariki nchi hizi zimepakana na bahari ya Hindi na upande wa kaskazini mashariki zimepakana na Somalia, upande wa kaskazini zimepakana na Ethiopia na Sudan Kusini upande wa magharibi ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na jamuhuri ya Rwanda na Burundi, kusini ni Zambia, Malawi na Msumbiji.

Nchi hizi zimepitiwa na mstari wa ikweta, umepita Kenya na kusini mwa Uganda. Kenya na Tanzania zina ukanda wa pwani wenye bandari za Mombasa; Tanga; Bagamoyo; Dar es Salaam; Zanzibar; Kilwa na Mtwara.


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira