Wizara ya Masuala ya Wanawake na Watoto
Wizara ya Masuala ya Wanawake na Watoto kwa kifupi (MWCA) au Wizara ya Jinsia, Watoto na Ulinzi wa Jamii kwa kifupi ni (MGCSP) ni Wizara ya Serikali ya Ghana inayohusika na uundaji wa Sera zinazokuza uanzishwaji na uhamasihsaji na maendeleo ya masuala ya Wanawake na Watoto.[1]
Historia
haririWizara hii iliundwa mnamo mwaka wa 2001 wakati wa utawala wa raisi John Kufuor kwa dhumuni la kushughulikia masuala ya wanawake na watoto.[1]
Mawaziri waliowahi kuhudumu MWCA na MGCSP
haririMkuu wa wizara hiyo ni Waziri wa Masuala ya Wanawake na Watoto na Waziri wa Jinsia, Watoto na Hifadhi ya Jamii. Mkuu wa kwanza wa wizara ilipoundwa mwaka wa 2001 alikuwa Gladys Asmah na mkuu wa kwanza wa wizara ilipobadilishwa jina na kuitwa MGCSP Februari 2013 ni Nana Oye Lithur. [2]
Year | Minister |
2001- 2005 | Gladys Asmah |
2005 - 2009 | Alima Mahama |
2009 - 2010 | Akua Sena Dansua (MP) |
2010 - 2012 | Juliana Azumah-Mensah (MP) |
2013 - 2017 | Nana Oye Lithur |
2017 - 2018 | Otiko Afisa Djaba |
2018 - 2020 | Cynthia Morrison (MP) |
Orodha hii hapo juu ni mawaziri walio wahi kuhudumu Wizara hiyo tangu ilipoanzishwa .
Mikakati na Malengo ya Wizara
haririmiongoni mwa malengo na mikakati ya Wizara ni kutunga Sera na miongozo juu ya maswala ya jinsia na watoto, kupendekeza programu zitakazokuza masuala ya Wanawake na Watoto na kuendeleza taasisi zinazohimiza na kuhamasisha harakati za uwezeshaji Wanawake.
Madhumuni
haririJukumu la wizara hiyo hulifanya ni kutetea matibabu bora kwa wanawake na watoto. Masuala ya kutia wasiwasi yanayojitokeza kwenye jamii dhidi wa Wanawake na Watoto hushughulikiwa na Wizara. Moja ya masuala hayo ni mwaka 2011 ambapo wizara ilitangaza kuwa ingeshirikiana na Idara ya Ustawi wa Jamii ya Ghana kufanya usajili upya wa vituo vyote vya watoto yatima nchini. Hii ilitokana na kuchapishwa kwenye vyombo vya habari kuhusu usimamizi mbovu wa baadhi ya Vituo vya watoto yatima nchini. Lengo kuu ilikuwa ni kuwaondoa wasio na leseni ya shughulu hizo kwenye mfumo. Machapisho hayo yaliripoti kwamba vituo vya watoto yatima vilikuwa vikitumika kama sehemu za kupitisha usafirishaji haramu wa watoto na vimekuwa mahali pa dhuluma na kumekuwa na unyanyasaji wa hali ya juu ndani ya majumba hayo.[3]
Tuzo
haririWizara mwaka 2011 iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake mjini Accra. Wakati wa kusherehekea Tuzo za kwanza za Wanawake wa Ghana waliobobea katika nyanja mbalimbali zilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Accra. Siku ya tuzo hizo ilikuwa na mada ya ‘Kumwezesha Mwanamke wa Ghana kwa Maendeleo ya Taifa’. Wanawake 34 wa Ghana walitunukiwa tuzo katika sherehe hiyo kwa michango yao mikubwa na inayoonekana kwa maendeleo ya kitaifa.[4]
Mafanikio
haririWizara kutoka 2001 imefanyia kazi masuala kadhaa yanayohusiana na hali wasiwasi kwa wanawake na watoto. Mambo hayo yanajumuisha kwenye mtiririko wa haya yafuatayo: [2]
- Kukomesha biashara haramu ya watoto
- Kuongeza idadi ya wanawake katika sekta kuu za serikali
- Kuelimisha wanawake kuhusu ukatili wa majumbani
- Uboreshaji wa sheria ya unyanyasaji wa majumbani
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 "Government Institutions". www.ghanaweb.com. Iliwekwa mnamo 2022-03-23.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-09-15. Iliwekwa mnamo 2022-03-23.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-04-30. Iliwekwa mnamo 2022-03-23.
- ↑ "Vice-Chancellor Honoured | About UCC". web.archive.org. 2011-07-23. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-23. Iliwekwa mnamo 2022-03-23.